Ninachotaka kuwambia ccm sasahivi wanatafuta kila mbinu ya kudhoofisha cdm
Minataka niwambie kuwa hadanganyiki mtu, na wameshemsha hapa hakuna mtoto wa kundanganywa kwa
ilo waelewe. Hata watafute uongo wao kutoka mbinguni 2015 watapata jibu lao la uongo
ata wafanyeje si wamezoea kuchakachua sasa achakachuliwi mtu, nataka niwambie 2015 itakuwa
jino kwa jino, shoka kwa shoka mpaka haki inapatikana tumewachoka hawa bubuzera na makhanga yao,
matisheti sasa niwakati wa kujikomboa. mpaka ukweli utajulikana na kujionesha wazi
Taifa litatikisika na itakuwa historia katika harakati za mageuzi.viongozi na wanachama wenye nguvu kwenye vyama mbalimbali vya siasa watafuata baadae.hatutamzuia mtu yeyote kujiunga na chama chetu.tuna timu kabambe ya kupokea na kuzungumza na makada na viongozi wa vyama mbalimbali wanaotaka kujiunga nasi.kwa kweli ni wengi sana
Tushirikiane katika ukombozi wa Taifa letu.Karibuni CHAUMMA.Propaganda chafu zinazoenezwa dhidi ya CHAUMMA ni mkakati wa kutunyonga.Tumekuja kukata kiu ya watanzania ya muda mrefu.Tangu taifa hili lipate uhuru hatujapata kuwa kuwa na chama kama hiki.Vijana karibuni kwa wingi na hivi punde tutazunguka nchi nzima sambamba na makongamano nchi nzima.Tutatumia usafiri wa anga na ardhini ili kurahisisha operation yetu nchi nzima
CHAUMMA kama ilivyo jina lake ni chama cha watu.Fursa ni kwa wote.Katika kanuni na katiba yetu hakuna kiongozi atakayekaa kwenye nafasi yake kwa zaidi ya vipindi viwili.Aidha apande ngazi ya juu,ya chini ama aondoke kwenye nafasi ili kutoa fursa kwa wengine kusukuma gurudumu la ukombozi.Tunaamini kama hatutaweza kuzingatia demokrasia ndani ya chama basi hatuwezi kulinda demokrasia na haki ya kijamii ndani ya Taifa letu.Karibuni
1-Ofisi zetu ziko Kijitonyama,karibu na soko la Makumbusho block no:45 plot No.376 Dar Es Salaam
Simu +255767977330,+255736502056,+255787623541
2-Katiba:Katiba ya chama ya mwaka 2012 na marekebisho yake yatakayofuata itakuwa ndiyo sheria mama na mwongozo au kanuni muhimu na jinsi ya kuendesha chama na masuala mbalimbali yanayohusu chama na asasi zake zote kama siyo idara zake
3-Bendera ya Chama:Itakiwa na rangi nne(4) kaa ifuatavyo:
Nyekundu:Maana yake ni ujasiri
Nyeupe:Inawakilisha amani na utulivu
Nyeusi:inawakilisha Bara la Afrika
Njano:inawakilisha wingi wa utajiri wa maliasili tuliyonayo nchini Tanzania
4:Nembo ya Chama:Itakuwa ni alama moja ambayo ni kiganja cha mkono kilicho kunjwa ikimaanisha umoja na mshikamano wa taifa letu,nembo hiyo itakuwa katikati ya bendera pamoja na maandishi ya kifupi cha jina la chama CHAUMMA katikati na maeneo yanayozunguka duara juu yasemayo CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA chini yake itakuwa mwaka wa chama kilipozaliwa(2012)
5:Itikadi ya chama(Ideology): Ni demokrasia ya kijamii ambayo misingi yake ni uhuru,umoja,ukweli,haki,amani,usawa mbele ya sheria,ustawi wa jamii na maendeleo kwa wote
6:Falsafa ya chama(philosophy):Umoja wa kitaifa,ukweli,uwazi,mshikamano na ujenzi wa jamii ya kidemokrasia iliyo huru na haki inayotendeke kwa wakati
7:Kauli mbiu ya chama(Slogan):Kibwagizo:CHAUMMA Kiitikio:''NGUVU YA MABADILIKO'' Lugha ya kiingereza ''CHAUMMA'' Kiitikio "POWER FOR CHANGE''
8:Msingi wa chama(foundation):Umma ndiyo chimbuko la mamlaka ya dolana maendeleo ya kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kijamii
9:Chama cha Ukombozi wa umma(CHAUMMA) kitakuwa na muundo ufuatao
i} Chemichemi:Ni ngazi ya chini na ya kwanza ya chama inayoundwa na wanachama wasiopungua watano(5) na wasiozidi kumi na Tano(15)
ii}Tawi:Ni ngazi ya pili ya chini na ya kwanza ya chama inayoundwa na chemichemi zisizopungua kumi(10) na zisizozidi thelathini (30) zilizoko kwenye tawi hilo
iii}Kata/Wadi:Ni ngazi ya tatu ya chini ya chama inayoundwa na matawi yasiyopungua matano(5) na yasiyozidi kumi na tano(15) yaliyoko kwenye kata hiyo
iv}Jimbo:Ni ngaziya kwanza ya kati ya chama ambayo na kata/wadi zisizopungua kumi(10) na zisizozidi ishirini na tano(25) kwenye jimbo hilo la uchaguzi
v}Mkoa:Ni ngazi ya pili ya kati ya chama ambayo inaundwa na majimbo yote ya uchaguzi yaliyoko kwenye mkoa huo
vi}Kanda:Ni ngazi ya tatu ya kati ya chama ambayo inaundwa na mikoa yote iliyomo kwenye kanda kama itakayogawiwa na halmashauri kuu ya taifa ya CHAUMMA