Vigogo CHADEMA wahusishwa na chama kipya - CHAUMMA

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Magazeti Leo Ijumaa

DSC_5198.JPG

DSC_5199.JPG

Hiki kiji-gazeti cha Hoja pamoja na kila cha Sauti Huru vinatia aibu kwa tasnia ya habari. Aibu aibu aibu ukisoma mambo wanayoandika humo ndani. Wengi wa waandishi wa hivi vijarida ni wanaume na ndio nashangaa wanaume gani wanandika umbeya kama huu?

Hoja wamezuka na CHAUMMA kuwa ni kimeanzishwa na CHADEMA! Nani asiyejua CCM ndio magwiji wa kuanzisha vyama vya msimu? Lakini pia hawa Hoja wamejikita sana kumshambulia Freeman Mbowe yeye binafsi kwa kusema kuwa 'DJ kuiongoza Tanzania kitakuwa kilele cha udhaifu'. Mbowe amekuwa kwenye siasa miaka 20 sasa imekuwaje leo ndio wanaona u-DJ wake? Hao ambao si ma-DJ wamefanya nini hii nchi?

Sauti Huru wao kazi yao ni moja - kuhubiri ukabila. Na waandishi wake ni wafanyakazi ofisi za CCM-Lumumba. Sijui CCM watajitoaje kwenye hii dhambi ya kugawa watanzania? Watapata wapi moral authority ya kusema wao ni chama cha watanzania wote na sio mafisadi? Wanataka watanzania wajikite kujadili ukabilia, udini ili wao CCM waendelee kuifasadi nchi?
 
Kijigazeti DHAIFU hakina hoja, kinatumiwa na mafisadi wa magamba ili kuchafua hali ya hewa ndani ya CHADEMA. Kama zilivyoshindwa propaganda za magamba katika kutaka kuonysha kwamba CDM ni chama cha wakristo na wachagga juhudi zao hizi kupitia hiki kijigazeti uchwara zitagonga ukuta.
 
Hili nalo ni gazeti la mafisadi! Hakuna jipya! Wameona chadema ina wapeleka mchakamchaka sasa ina bidi waunde viabari vya kizushi.

Hatudanganyiki na hii ndio chorus yao mpya! Madaktari waligoma wakasema cdm, sasa kachama njaa wame kaanzisha wanasema cdm!

Tunajua na walimu wakigoma mtasema cdm. Na hii ndio ishara ya kushindwa kwa serikali dhaifu ya jk, kila kukicha ni kutafuta mtu wa kumtupia udhaifu wa serikali yake.
 
Siwezi kupoteza muda kushabikia habari za magazeti ya uamsho kwani haya magazeti dhaifu kama haya yote akili zao ni sawa na radio iman au gazeti al-nuur kwani yote kwa pamoja yanandikwa kwa kutumia ukilaza, kwani huwezi eti hii habri kuiamini kwani imekaa kiudaku zaidi pia inatumia jina la CDM kujiuza.
 
system at work. Habari hizo hazitutishi sisi cdm tupo imara kabisa. Peoplesssssssssssss
 
Hiki kiji-gazeti cha Hoja pamoja na kila cha Sauti Huru vinatia aibu kwa tasnia ya habari. Aibu aibu aibu ukisoma mambo wanayoandika humo ndani. Wengi wa waandishi wa hivi vijarida ni wanaume na ndio nashangaa wanaume gani wanandika umbeya kama huu?

Hoja wamezuka na CHAUMMA kuwa ni kimeanzishwa na CHADEMA! Nani asiyejua CCM ndio magwiji wa kuanzisha vyama vya msimu? Lakini pia hawa Hoja wamejikita sana kumshambulia Freeman Mbowe yeye binafsi kwa kusema kuwa 'DJ kuiongoza Tanzania kitakuwa kilele cha udhaifu'. Mbowe amekuwa kwenye siasa miaka 20 sasa imekuwaje leo ndio wanaona u-DJ wake? Hao ambao si ma-DJ wamefanya nini hii nchi?

Sauti Huru wao kazi yao ni moja - kuhubiri ukabila. Na waandishi wake ni wafanyakazi ofisi za CCM-Lumumba. Sijui CCM watajitoaje kwenye hii dhambi ya kugawa watanzania? Watapata wapi moral authority ya kusema wao ni chama cha watanzania wote na sio mafisadi? Wanataka watanzania wajikite kujadili ukabilia, udini ili wao CCM waendelee kuifasadi nchi?
Mkuu kwani mtu akiwa anamiliki mabasi kwani lazima awe konda au utingo? Au wale wanaomiliki kampuni za ulinzi pia wao ni walinzi pia na uhakika wanaomiliki kumbi za starehe siyo mabaunsa au madj Kama Hilo gazeti linavyoripoti
 
Rais dhaifu, serikali dhaifu,chama dhaifu, spika dhaifu,wabunge dhaifu,mbinu za kuibomoa Chadema nazo dhaifu. Upuuzi mtupu, habari hizi hata mtoto wa chekechea hawezi kuziamini. Watanganyika tukatae udhaifu kwa kuipiga chini CCM.
 
Ama kweli serikali dhaifu inatumia mbinu dhaifu kukabiliana na chama imara CDM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom