Vigogo Chadema wahamia CCM

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi kimepata pigo la kuondokewa na viongozi wake wawili, akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya,Hassani Mkopi na katibu wake,Saadati Kamalu.

Viongozi ambao wameachia ngazi na kujiunga na CCM kwa madai ya kushindwa kukitumikia vema chama hicho tangu walivyokabidhiwa madaraka kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Katibu wa muda wa Chadema, Jordani Membe alisema juzi kuwa Mkopi alijiondoa Chadema na kujiunga na CCM mwishoni mwa mwezi uliopita wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal katika Kijiji cha Chiumbati, Kata ya Naipanga.

“Tukiwa katika mkutano huo katika Kijiji cha Chiumbati, ghafla mwenzetu aliamua kujivua gamba la Chadema na kulivaa lile la CCM kwa kumpatia Dk. Bilal kadi yetu ya Chadema,” alisema Membe.

“Katibu wetu Kamalu amedai ameamua kujiuzulu baada ya kushindwa kukitumikia vema
chama kama alivyokabidhiwa na wanachama wakati wa uchaguzi uliopita,” alisema akinukuu kauli yake.

Kutokana na kujiuzulu kwa Kamalu, Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na Baraza la Wazee wa Chadema waliamua kufanya uteuzi mdogo wa kuziba nafasi hiyo, ambapo Diwani wa Kata ya Nkotokuyana, Likolovero Hassani alichaguliwa nafasi ya uenyekiti, na yeye Membe aliteuliwa kushika nafasi ya ukatibu wa muda.

Membe alisema viongozi hao watashikilia nafasi hizo hadi Uchaguzi Mkuu wa Chadema utakapofanyika mwaka 2013, badala ya 2014 kutokana na mabadiliko mafupi yaliyofanyika kwa lengo la kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za vijiji, vitongoji na mitaa

HABARILEO

Naelewa mashabiki wenzangu hampendi kuona hii,lakini ndio uhuru wa habari ulivyo
 
Huu upuuzi mwingine unakera.Hii habari imetolewa hapa wiki tatu zilizopita.Leo gazeti la propaganda la ccm linaona ndio habari kuu.Huu ni upofu.
 
CHADEMA haijawahi kuwa na viongozi wa wilaya huko Nachingwea. acheni kutafuta sifa za kijinga
 
Source Habarileo, hivi hata viongozi huko Nachingwea (kama waliwahi kuwapo) nao vigogo? Hao si vijiti tu.
 
Mtoa mada acha ushabiki hivi unajua maana ya kigogo, ukisema vigogo CDM wahamia CCM unatakiwa umananishe viongozi makao mkuu na tena wenye influence.
 
Njaa ni mwanaharamu...mimi nasema kama kuna mtanzania anatoka chama chochote cha upinzania na kujiunga CCM anahitaji matibabu ya ubongo..Lakini pia kama kuna mtanzania ambaye hana chama kwa sasa na anafikiria kujiunga CCM anahitaji matibabu haraka ya ubongo.
 
Source Habarileo, hivi hata viongozi huko Nachingwea (kama waliwahi kuwapo) nao vigogo? Hao si vijiti tu.

ni vyema mkafuatilia na kujuwa nini tatizo,kuliko kupiga kelele bila kuweka mambo sawa,
 
Mtoa mada acha ushabiki hivi unajua maana ya kigogo, ukisema vigogo CDM wahamia CCM unatakiwa umananishe viongozi makao mkuu na tena wenye influence.

we pambana na HABARILEO sio mimi,nimetimiza wajibu juu ya kuhabarishana yaliyobaki ni wewe na mwandishi na sio mweka post
 
Kuna wachumia tumbo wengi sana, hao waliingia cdm wakifikiri kuna mianya ya kula pesa za walipa kodi, wakakuta hakuna uwezekano wa kupata mianya hiyo. Waangalieni kwa makini sana hao wanaohamia ccm toka cdm. Vilevile kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina kwa wanaogombea nafac mbalimbali cdm. Kuna wengine ni mamluki lengo lao ni kutaka kubomoa chama pindi wakiwa na influence ndani ya chama kwa kurudisha kadi kwnye mikutano ya hadhara!
 
... watakua wamewezeshwa kilo ngapi ya ngawira? Si kila mtu anayo uwezo wa kuona mabadiliko nchini yanakoelekea hadi hivi sasa; waacheni kidogo wakatalii huko wakigundua walivyopotea watarudi wenyewe tu!!
 
Mtoa mada acha ushabiki hivi unajua maana ya kigogo, ukisema vigogo CDM wahamia CCM unatakiwa umananishe viongozi makao mkuu na tena wenye influence.

Propaganda zingine bwana zinasikitisha sana. No objectivity at all.
 
Back
Top Bottom