Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
:
Katika hali isiyotarajiwa, viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya uwepo wa taarifa zinazodai kuwa wamefunguliwa kesi nyingine ya jinai kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakidaiwa kukiuka amri ya Mahakama iliyotolewa Juni 10.2025
Inatajwa kuwa amri inayodaiwa kukiukwa inatokana na maamuzi ya Mahakama ya maombi Na. 8960/2025 ambayo msingi wake ni wa kesi ya madai Na. 8323/2025 iliyofunguliwa Mahakamani hapo na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed, Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, kesi iliyopo mbele ya Jaji Hamidu Mwanga
Taarifa ilizozipata Jambo TV kutoka kwenye vyanzo vyake vya kuaminika imeonesha kuwa maombi hayo yamefunguliwa na waleta maombi kwenye kesi ya msingi ambao ni Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2), ambapo vigogo wa CHADEMA wanaodaiwa kukiuka amri hiyo ni pamoja na John Wegesa Heche (Makamu M/Kiti Tanzania Bara), Amani Golugwa (Naibu K/Mkuu Tanzania Bara), Godbless Lema (Mjumbe wa K/Kuu), John Pambalu (Mkurugenzi wa Organization) na Boniface Jacob (M/Kiti Kanda ya Pwani na Mjumbe K/Kuu),
Wengine ni Pamela Maassay (K/Mkuu BAWACHA), Hamad Mussa Yussuf (Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi Z'bar), Gervas Lyenda (Mkuu wa Idara ya Habari), John John Mnyika (Katibu Mkuu), Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Kesi hiyo itakuwa ni ya pili kufunguliwa kwa vigogo wa CHADEMA, kesi ya kwanza kama hiyo ilitupiliwa mbali baada ya Mahakama kupitia Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kukubaliana na hoja za upande wa utetezi kuwa waleta maombi walifungua kesi nje ya muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria...