Vigezo vya kuweka biashara yako supermarket

mimi ni mimi

Senior Member
Nov 2, 2012
122
225
Habari zenu waungwana,

Mimi ni binti niliyeolewa mwaka huu. Awali nilikuwa nafanya kazi kwenye moja ya NGO hapa jijini Dar mpaka pale tulipopunguzwa kazini kutokana na hali ya uchumi wa kampuni kuyumba.

Nimekaa nyumbani nikiwa najaribu kutafuta ajira nyingine kwa miezi kadhaa sasa bila mafanikio ili niweze kumsapoti mwenzangu katika kuendesha maisha. Ndipo nimefikia uamuzi wa kuangalia upande mwingine wa shilingi.

Ninaujuzi wa kutengeneza bites tofauti tofauti na nzuri. Nimejaribu kutembelea maduka ya jirani ili nipeleke biashara yangu; maduka mengi kuna bites tayari na sijaona kama yamekaa kwenye eneo zuri la bidhaa kununuliwa kwa haraka. Sasa nimepata wazo la kupeleka supermarkets na kujitangaza kwa njia ya mtandao. Je kuna vigezo vinavyozingatiwa ili kupeleka bidhaa huko? Kama vipo ni vipi?

Nawasilisha.
 

Cowman

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
1,640
2,000
Ww unaproduce katika smallest scale dada yangu kule supermarket watakuzingua tu halafu watakwambia wananunua kwa credit after 30-60 days. Jaribu kuuza wewe mwenyewe direct kwa customers. Tafuta vijana watembeze mitaani, waweza peleka shule za msingi pia
 

momo2

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
429
500
Kitu kingine ambacho unaweza kufanya ni kutafuta frame na kuweka kama biashara yako ukaweka bites na soft drinks,fresh juice uku ukitoa tangazo lako kwenye mitandao ya kijamii,pambana uweze kufanya delivery maofisini maana watu wengine wanaenda kazini mapema na wanaitaji bites za kunywea chai.
 

mtafutaji2016

Senior Member
Jun 19, 2016
108
225
Kitu kingine ambacho unaweza kufanya ni kutafuta frame na kuweka kama biashara yako ukaweka bites na soft drinks,fresh juice uku ukitoa tangazo lako kwenye mitandao ya kijamii,pambana uweze kufanya delivery maofisini maana watu wengine wanaenda kazini mapema na wanaitaji bites za kunywea chai.
Gud idea hasa akipata location nzur.
 

Erick B

Senior Member
May 25, 2017
108
225
Tembelea super market watakupa maelezo ya uhakika zaidi and all requirement... pambana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom