mimi ni mimi
Senior Member
- Nov 2, 2012
- 129
- 51
Habari zenu waungwana,
Mimi ni binti niliyeolewa mwaka huu. Awali nilikuwa nafanya kazi kwenye moja ya NGO hapa jijini Dar mpaka pale tulipopunguzwa kazini kutokana na hali ya uchumi wa kampuni kuyumba.
Nimekaa nyumbani nikiwa najaribu kutafuta ajira nyingine kwa miezi kadhaa sasa bila mafanikio ili niweze kumsapoti mwenzangu katika kuendesha maisha. Ndipo nimefikia uamuzi wa kuangalia upande mwingine wa shilingi.
Ninaujuzi wa kutengeneza bites tofauti tofauti na nzuri. Nimejaribu kutembelea maduka ya jirani ili nipeleke biashara yangu; maduka mengi kuna bites tayari na sijaona kama yamekaa kwenye eneo zuri la bidhaa kununuliwa kwa haraka. Sasa nimepata wazo la kupeleka supermarkets na kujitangaza kwa njia ya mtandao. Je kuna vigezo vinavyozingatiwa ili kupeleka bidhaa huko? Kama vipo ni vipi?
Nawasilisha.