Kuwa Kinara Sokoni (Being The Market Leader) Bila Kufanya Matangazo

Feb 5, 2022
31
48
1662739266528.png

Mara nyingi ninapokutana na wamiliki au wakurugenzi wa makampuni (Business Executives), huwa nawauliza ni njia ipi huwa wanatumia kujijenga sokoni "market leading branding" wengi wanasema kufanya matangazo (advertising) ndio njia muafaka, kwa sababu; matangazo hujenga uelewa wa huduma au bidhaa kwa wateja, pia ni njia ya mawasiliano kati ya kampuni na mteja.

Kupitia makala haya, nitapenda kuja na mtazamo tofauti juu ya ujengaji wa "brand" ya bidhaa au huduma zako sokoni. Kuna kampuni nyingi zimekuwa zikiongoza mauzo sokoni pasina kuweka nguvu kubwa kwenye matangazo.
Ili kujenga "brand" pasina kufanya matangazo, zingatia yafuatayo;
  • Chagua soko la watu wengi (mass market) na hakikisha unakuwa na idadi ya kutosha ya bidhaa (having enough volume of products). Kuhudumia soko la watu wengi (mass market) maana yake ni kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya wateja wengi kwa wakati mmoja (fulfil mass customers' expectation at at time). Wafanyabiashara wa reja reja (retailer traders) mara nyingi hawapendi kufanya kazi na kampuni ambazo hazina uwezo wa kupeleka bidhaa nyingi kwa wakati mmoja sokoni.
  • Zingatia ubora wa bidhaa zako. Miongoni mwa malengo ya "branding" katika biashara ni kufuta/kupunguza dhana hasi juu ya ubora wa bidhaa kwa mteja (reduce perceived risk to the consumers). Hivyo basi, hakikisha wakati wote mteja anapotumia bidhaa yako, anapata ubora ule ule kama aliopata jana na juzi.
  • Uza bidhaa zako kwa bei ya chini. Kimsingi, hii ni kanuni kwenye soko la watu wengi (mass market). Ili ufanikiwe katia hili, hakikisha gharama zako za uzalishaji (production cost) zinakuwa chini kadiri iwezekanavyo (ZINGATIA, gharama zisiwe chini sana kiasi cha kufanya bidhaa zako kukosa ubora)
  • Kwa bidhaa za vinywaji, fahamu ladha (taste) inayopendwa na wateja uliowalenga, kisha tengeneza vinywaji venye ladha inayokubalika na kupendwa na wateja hao, pia hakikisha unamlenga mlaji wa mwisho sokoni (you should be driven by end-users)
  • Ingia makubaliano na wauzaji wa reja reja, ili wakuuzie bidhaa zako (make agreements with multiple retailers).
AHSANTE
OMAR MSONGA (BA.PPM & CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Back
Top Bottom