Kutembeza biashara kuna kuaunderrate muuzaji(hivi wateja mnawachukuliaje(chinga)?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,995
Habari zenu

Leo ni siku nyingine tunamshukuru Mungu kwa kuliona jua hadi sasa lakini pia kwa neema ya kuona mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ndugu zangu waislamu lakini kwa wakristo nadhani bado mnaendelea kufunga.

Ndugu zangu kitaa kigumu sana,kazi zimekuwà ngumu kupatikana kwa sisi tuliosomaa na hakuna konekisheni wengi wetu, tumeamua kujiajiri kupitia biashara lakini bado changamoto ni kubwa mno.

Tunatembeza biashara ili kuleta urahisi wa kuuzika bidhaa pamoja na kujitangaza lakini kwa bahati mbaya madada na makaka tunaowauzia bidhaa wanatuonea na kutuchukulia tofauti.

1_Njaa kali
2_Wakuja
3_Malofa na wajinga

Unaweza kupeleka bidhaa na kuongea naye fresh dakika za mwisho"sina pesa", "unapunguzaje", "bei kubwa" n.k.

Nashauri

Ikiwa unataka kuanza kufanya biashara tafuta sehemu ya kufanya ili uipe heshima biashara yako huenda utapunguza zile panga za bei coz bidhaa hyo unayouza ukienda madukani bei imesimama hivo hivo ila kwa kuwa unatembeza inashuka thamani.

Wasalamu.
 
Hii ishu ya kutembeza hutokana na mtaji ulio nao lakini kiukweli ni bora utembeze tu.
Yupo atayekuunga amini kwamba utauza tu licha ya kuwa wanao kudharau wapo kikubwa ni kukaza roho ili usife njaa na kukosa chochote kitu.

Mimi niliwahi tembeza nguo za watoto tena mtumba kwa mtaji usiozidi elfu kumi na tano. Still nilisurvive mpaka nilipopata deal lingine. hizi biashara za kutembeza faida zake huwa ndogo ila pia hutegemea na utembezaji wako na uchap pia...
 
Ni nzuri kwa mtaji mdogo hii biashara wala msiogope wanunuzi wapo, kujiamini kutawatoa. Unacho pata save.
Mfano uuzaji wa eye phones, betri za simu, memory na flash n.k mtaji wake ni 20,000.

Suruali za wadada za tight na jeans za kupoint nzuri mtaji wake pia ni 20,000.
Hata uwe na chini ya 20K unafanya kibishi kuliko kupiga mihayo.
Viatu vya mtumba mtaji ni 30,000 mpaka 50,000 zile raba kali.

Vifaa vya mazoezi mtaji ni amsini kama kamba za kuruka zile.
Kuna jamaa hapo juu ni mchagga mwenzangu kasema kuna vyombo kama chupa za chai, sufuria na vijiko ila najua hivi mtaji ni mkubwa kidogo kama laki hivi, au chini ya 80K.
Niliwahi kaa mkoa mgumu saidia fundi ikigoma nilichobakisha nafanyia uchinga, wale wanao remba wadada kucha ukiwa smart unapiga pesa sema chunga sana kuwafuata wadada makwao, labda makazini kwao.
 
Dah msinikumbushe. Kuna nyumba nilienda wapangaji shazi waliniweka dakika zaidi ya 60 hamna alienunua ata kitu.

Kuna house nilienda pia ya kishua flani maza alinunua afu akanipa maji ya kunywa, the way alivoona nayafakamia, akajua uyu hajala, akanipa chapati, ilikua mida ya saa 8 mchana aisee, inaweza kua chapati iliobaki asubuhi angeitupa, ila alisevu a day.

Mapambano yaendelee wakuu
 
Back
Top Bottom