Vigezo vilivyotumika kumpa nishani speaker wa sasa!

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Kwenye sherehe hizo pamoja na kutunuku Msekwa na Makinda wengi wamejiuliza sababu za kutoswa kwa ‘Spika wa Bunge la Kasi na Viwango', Samuel Sitta.

Baadhi ya wanasiasa wazoefu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha maspika hao kutunukiwa nishani na Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuachwa.

Mmoja wa wanasiasa hao kutoka CCM ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema huenda Sitta hakupewa zawadi kutokana na chama hicho tawala kumtuhumu kuwa anaongoza makundi ya upinzani ndani ya chama, jambo ambalo mara kadhaa mwanasiasa huyo amekuwa akilikanusha.

Alisema huenda kutokana na msimamo wake imara usioyumba wa kupambana na vitendo vya ufisadi bila woga ndilo jambo ambalo linalokera wenzake ndani ya chama hicho nakutafsiri kwamba ni kukigawa chama .

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema hajui vigezo vilivyotumika kutoa nishani hizo lakini yeye anaamini Sitta aliweza kulifanya Bunge kuendesha mambo kiuwazi kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kuwa na imani nalo.

"Alisema tangu awali Bunge lake litakuwa la ‘standard and speed' (kasi na viwango ) na liliweza kuonyesha hilo… lakini mimi Napata kigugumizi cha kusema sababu sijui vigezo vilivyotumika," alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na alihudhuria sherehe hizo.

Alisema ingawa yeye alichelewa kufika kwenye sherehe hizo, alishangazwa kusikia kuwa Makinda amepata tuzo hiyo wakati kipindi chake cha uspika hakijamalizika.

Spika mwingine ambaye hakutajwa kwenye orodha hiyo ni Yule aliyekuwa wa kwanza baada ya Tanzania kupata uhuru, Chifu Adam Sapi Mkwawa (1964-1973 na 1975-94) na Erasto Mang'enya (1973-75).

Nishani ya juu kabisa iliyotolewa ni ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo walitunukiwa maraisi wa awamu zote tatu zilizopita, Hayati Mwalimu Nyerere ambayo ilipokelewa na Mama Maria Nyerere kwa niaba yake, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Source<Mwananchi Jpili
MY TAKE>
Mtu hutunukiwa nishani based on his or her workdone/accomplished duties sasa huyu speaker wa sasa ndo kwanza ana Mwaka tuu kwenye icho kiti akiboronga in 4 years time atanyanganywa iyo Nishani.
Naona tunaendelea kuuishi ule usemi usemao TZ we are not serious in everything being a reflection of the current regime.
 
Hizo tuzo zilidhaminiwa na Rostam Azizi kwahiyo kwa namna yoyote ile usingetarajia Sitta kuwa mpokeaji.
Si kweli basi kama hivyo EL angepata, lakini cha ajabu hata Adamu Sapi spika wa kwanza hakupata kapewa Makinda ambaye hajamaliza hata mwaka lini wamepima utendaji wake na matokeo (outcomes).
 
Nami nilikua na wazo hilohilo,kama mdhamin ni R.A,basi E.L angepata ya heshma kama Nyerere,ila sasa nachokiona sasa ndo ile UTAK0MA,WE C MJANJA NTAKU0NYESHA,NDO MI NAONA WANAONESHANA
Si kweli basi kama hivyo EL angepata, lakini cha ajabu hata Adamu Sapi spika wa kwanza hakupata kapewa Makinda ambaye hajamaliza hata mwaka lini wamepima utendaji wake na matokeo (outcomes).
 
Labda kwa kuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa spika wa bunge letu!
 
Si kweli basi kama hivyo EL angepata, lakini cha ajabu hata Adamu Sapi spika wa kwanza hakupata kapewa Makinda ambaye hajamaliza hata mwaka lini wamepima utendaji wake na matokeo (outcomes).

EL asingeweza kupokea kwasababu hakuwa na sababu za kupewa.
 
mi huwa nashangaa,EL kila siku anajitangaza ni rafiki wa JK,mbona JK huwa hajitangazi ni rafiki wa EL?
 
Nishani ka tuzo za KILL music(kili music awards),zinazodhaminiwa na Knjaro
 
Atakuja raisi ambaye atakuja weka mambo sawa msihofu ivi vijembe na fitina wanazopigana hawa viongozi wetu zina mwisho wake.
 
Back
Top Bottom