Vifo vya watoto usingizini: Uchawi au ujinga…?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
111125080826-african-american-baby-infant-sleeping-back-story-top.jpg

Hivi karibuni umetokea msiba wa mtoto wa miezi miwili maeneo ninapoishi. Mtoto huyo alifariki ghafla akiwa usingizini. Mama wa mtoto huyo aliamka asubuhi na kukuta mwanaye amefariki. Wakati tunandaa mazishi, nilisikia minong'ono juu ya kifo cha yule mtoto kuhusishwa na imani za kishirikina na mlengwa alikuwa ni bibi mmoja anayeishi hapo mtaani. Ile minong'ono iliendelea hadi tukazika, na kila mtu kuendelea na shughuli zake. Vifo vya ghafla vya watoto chini ya mwaka mmoja huwa vinatokea sana, ingawa hakuna takwimu sahihi kwa sababu watu huwa wanazika kimyakimya, bila watoto hao kufanyiwa uchunguzi kitaalamu ili kujua sababu ya kifo cha mtoto huyo.

Huenda hata wewe unayesoma hapa utakuwa shahidi yangu kuwa pia umewahi kusikia au kushuhudia kifo cha ghafla cha mtoto wa chini ya mwaka mmoja. Na bahati mbaya zaidi vifo hivyo vimekuwa vikihusishwa na imani za kishirikina. Familia nyingi zimesambaratika na wengine wameuawa kwa kuhusishwa na vifo vya namna hii. Lipo tatizo ambalo linafahamika kama Sudden Infant Death Syndrome (SIDS), ambalo kwa Marekani hujulikana kama Crib Death. Hiki ni kifo cha ghafla cha mtoto wa chini ya mwaka mmoja ambapo sababu ya kifo inakuwa haifahamiki, pengine hata baada ya uchunguzi wa mwili wa mtoto kufanyika.

Tatizo hili ndilo linalosababisha vifo vya watoto wengi wa umri chini ya mwaka mmoja, na siyo kwa Tanzania pekee bali duniani kote. Kwa mfano Marekani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2009, ilionyesha kwamba watoto wapatao 2,226 walifariki kutokana na tatizo hilo. Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu za nyuma inaonyesha kwamba idadi hiyo imepungua kwa asilimia 50, na hiyo ilitokana na kampeni iliyoanzishwa nchini humo iliyopewa jina la Back-to-Sleep Campaign ambayo ilizinduliwa mwaka 1994. Hiyo ni Marekani ambapo wenzetu wametutangulia kwa teknolojia ya utabibu. Naamini kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi.

Kwenye kitabu cha Molecular Link Between the Sudden Infant Death Syndrome and the long- QT Syndrome, pamoja na jarida la Medical Association la Oktoba 2006 inaonekana kwamba, watoto wengi wanaofariki kwa vifo vya namna hii, wale wa kiume wanaongoza kwa asilimia 61, ukilinganisha na watoto wa kike. Imebainika kwamba, watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya ubongo kwa upande unaohusika na upumuaji ambapo pia vifo hivi vinahusishwa na sababu za kizalia (genetic), ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja.

Zipo sababu nyingi mbazo zinahusishwa na kuzaliwa kwa watoto wanaokumbwa na vifo vya ghafla usingizini ambazo baadhi yake ni hizi zifuazo:

-Mama mzazi kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito
-Mama mjamzito kutopata vyakula vyenye virutubisho.
-Mimba za utotoni
-Mama kuzaa haraka haraka bila kupata muda wa kupumzika baada ya kujifungua
-Mama mjamzito kuvuta sigara
-Mama mjamzito kutumia madawa ya kulevya au pombe kupita kiasi
-Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.

Sababu nyingine inayotajwa mbali na hizo hapo juu ni ile inayotokana na ulalaji wa mtoto. Inawezekana mtoto akazaliwa akiwa na afya yake njema, lakini anaweza kupatwa na kifo cha ghafla usingizini kutokana na namna alivyolazwa. Kwa mfano kumlaza kifudifudi mtoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja kunahusishwa na vifo vya namna hii, lakini pia hata kumlaza kiubavu nayo si salama, kwani ni rahisi sana mtoto kugeuka mwenyewe na kama ikitokea amejiziba pumzi ni rahisi kupoteza maisha. Inashauriwa kama mtoto analazwa kifudifudi asilazwe kwenye godoro laini mto laini au blangeti laini kama sufi, kwani ni rahisi kusababisha joto na kumfanya mtoto kuvuta hewa yenye joto na hivyo kumsababishia kifo. Inashauriwa mtoto wa umri huo kulazwa chali, kwani ulalaji wa namna hiyo ni salama na ndio sababu Marekani walianzisha kampeni ya kuwahimiza kina mama kuwalaza watoto wa chini ya mwaka mmoja chali na wakafanikiwa kupunguza vifo vya ghafla kwa watoto wa umri huo kwa asilimia 50.

Pia mama kumnyonyesha mtoto huku akiwa amelala husababisha vifo vya ghafla. Inashauriwa mama anapomnyonyesha mtoto awe amekaa kwani akimnyonyesha huku akiwa amelala anaweza kupitiwa na usingizi na kusababisha mtoto kuzibwa pumzi na ziwa la mama na hivyo kupoteza maisha. Uvutaji wa sigara karibu na mtoto na kumlaza mtoto katika chumba kisicho na hewa ya kutosha huweza kusababisha kifo cha ghafla kwa mtoto huyo.

Kwa hiyo basi, vifo vingi vya ghafla vya watoto wa umri huu, ambavyo vinahusishwa na imani za kishirikina, vikichunguzwa sana, itagundulika kwamba, sababu nilizozitaja, zinahusika moja kwa moja. Lakini kwa sababu ya kutojua, watu wanakimbilia kushikana uchawi. Ni vyema kama mama wajawazito wataelimishwa kuhusu tatizo hili na sababu zinazosababisha pale wanapohudhuria kliniki ili wachukue tahadhari.
 
Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,239
1,225
John Santrock katika kitabu chake "Life-Span Development" anaeleza kuwa SIDS uwapata zaidi watoto wachanga wenye umri wa wiki 4 mpaka 6. research nyingi pia zinaonyesha kuwa pamoja na sababu zilizotajwa na mtambuzi, zifuatazo nazo zinachangia kutokea kwa hivi vifo vya gafla vya vichanga: mtoto kuzaliwa na uzito mdogo; mtoto kuwa exposed katika sigara au vilevi vya kuvuta(si lazima Mama avute, ata baba au mtu yeyote anapovuta karibu na mtoto); mtoto kulazwa kwenye matandiko laini. etc.

Mwandishi huyo aneleza pia hivi vifo vya ghafla vya vichanga vinahathiri zaidi watoto waliozaliwa ndani ya familia zenye hali duni kiuchumi (low socio-economic) pengine hii ni kwa sababu wengi wao hawana elimu ya kutosha juu ya namna ya kutunza na kukuza watoto, pengine ni kwa sababu makazi yao yanakuwa congested kiasi kwamba hakuna hewa ya Oksijeni ya kutosha hasa nyakati za usiku, pamoja na uchafu uliyokithiri na mfumo mzima wa lishe kutokuwa bora!

Kimsingi SIDS siyo uchawi, wazazi waache kuwafunga watoto wao mairizi makubwamakubwa, wazingatie lishe, usafi, na kufata taratibu sahihi za kiafya!
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,988
2,000
Out of Topic may be:

Nikiwa mdogo niliwahi kushuhudia mtoto akifa akiwa mikononi mwa Bibi mmoja jirani.
Mimi na mwenzangu tulikuwa tumesimama pembeni (nafikiri mpira wetu ulidondokea mahali alipokaabibi yule).
Wakati tunamtizama mara mtoto akaanza kubadilisha macho............Kilichofuata ni bibi kumuita Mama mwenye mtoto
na kuanza kulia.

Yule bibi alipata wakati mgumu sana kwa sababu huko nyuma alikuwa na tuhuma za ulozi

Siwezi kusahau ilitokea natizama kwa macho yangu mawili.
 
Unayoyasema kuhusu hali duni ya uchumi na makazi duni kusababisha vifo vya aina hiyo nakubaliana na wewe.
Nakumbuka miaka ya 80 wakati naisha Mwananyamala vifo vya wa watoto wachanga vilikuwa vinatokea sana na watu walikuwa wanashikana uchawi ile mbaya.

Baada ya kusoma huo utafiti ndio nikagundua kwamba ule ulikuwa ni ujinga tu. Kunahitajika elimu hii itolewe wakati kina mama wanapohudhuria kliniki............
 
Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,239
1,225
Nakubaliana nawe juu ya haja ya kutoa elimu; Naamini kuna Madaktari, waganga na wahudumu wa afya wako humu JF, basi tuwape changamoto ya kuhakikisha hii elimu wanaipata wamama wajawazito/wenye vichanga wanapohudhuria kliniki zao!Unayoyasema kuhusu hali duni ya uchumi na makazi duni kusababisha vifo vya aina hiyo nakubaliana na wewe.
Nakumbuka miaka ya 80 wakati naisha Mwananyamala vifo vya wa watoto wachanga vilikuwa vinatokea sana na watu walikuwa wanashikana uchawi ile mbaya.

Baada ya kusoma huo utafiti ndio nikagundua kwamba ule ulikuwa ni ujinga tu. Kunahitajika elimu hii itolewe wakati kina mama wanapohudhuria kliniki............
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
Out of Topic may be:

Nikiwa mdogo niliwahi kushuhudia mtoto akifa akiwa mikononi mwa Bibi mmoja jirani.
Mimi na mwenzangu tulikuwa tumesimama pembeni (nafikiri mpira wetu ulidondokea mahali alipokaabibi yule).
Wakati tunamtizama mara mtoto akaanza kubadilisha macho............Kilichofuata ni bibi kumuita Mama mwenye mtoto
na kuanza kulia.

Yule bibi alipata wakati mgumu sana kwa sababu huko nyuma alikuwa na tuhuma za ulozi

Siwezi kusahau ilitokea natizama kwa macho yangu mawili.

Imebainika kwamba, watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya ubongo kwa upande unaohusika na upumuaji ambapo pia vifo hivi vinahusishwa na sababu za kizalia (genetic), ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja.
Kama nilivyoeleza hapo juu kwamba wapo watoto ambao huzaliwa na matatizo ya kwenye ubongo kwa upande unaohusika na upumuaji au matatizo ya kizalia (genetic).
Nashindwa kushawishika moja kwa moja na imani za kishirikina kwa sababu hata huko Marekani ambapo imani za kishirikina hazina nafasi kama ilivyo kwetu, tatizo lilikuwa ni kubwa sana pamoja na kuwa na teknolojia ya hali ya juu ya utabibu. Ni pale tu walipoanzisha kampeni ya Back-to-Sleep ndipo walipofanikiwa kupunguza idaidi ya vifo hivyo..............
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
Nakubaliana nawe juu ya haja ya kutoa elimu; Naamini kuna Madaktari, waganga na wahudumu wa afya wako humu JF, basi tuwape changamoto ya kuhakikisha hii elimu wanaipata wamama wajawazito/wenye vichanga wanapohudhuria kliniki zao!

Nakubaliana na wewe mkuu, na mtu kama Dr. Riwa anahusika sana.............
 
Last edited by a moderator:

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,239
1,225
Mkuu kinachoelezwa hapa ni Vifo vya Watoto wachanga Vinavyotokea wakIWA USINGIZINI hasa nyakati za USIKU,
ambayo katika hali ya kawaida inasababishwa na ukosefu wa hewa ya oksijeni yakuosha.

Ni ngumu sana kwa raia wa kawaida kukuelewa kwa sababu fikra za waafrika walio wengi zimetawaliwa na ushirikina, ndo mana hata katika sehemu za kazi, wengi wanaamini katika uchawi ili kuendelea kubaki na nyadhifa zao badala ya kuamini katika utendaji (out of topic though).

Maneno matakatifu yanasema: "..Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.."

Out of Topic may be:

Nikiwa mdogo niliwahi kushuhudia mtoto akifa akiwa mikononi mwa Bibi mmoja jirani.
Mimi na mwenzangu tulikuwa tumesimama pembeni (nafikiri mpira wetu ulidondokea mahali alipokaabibi yule).
Wakati tunamtizama mara mtoto akaanza kubadilisha macho............Kilichofuata ni bibi kumuita Mama mwenye mtoto
na kuanza kulia.

Yule bibi alipata wakati mgumu sana kwa sababu huko nyuma alikuwa na tuhuma za ulozi

Siwezi kusahau ilitokea natizama kwa macho yangu mawili.
 
Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
0
Huo utafiti niliusoma na kuuelewa vyema mwanangu akiwa na wiki moja tu. Nikashauriana na mkr wangu kuwa mtoto tusimlaze tena kwa tumbo.
Baadae mwanetu akaanza kusimbuliwa na tumbo kujaa gesi, tukaambiwa eti ni kwa sababu ya namna tunavyomlaza. Je kuna uhusiano wowote kati ya mtoto anavyolala na tumbo kujaa gesi?
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
Huo utafiti niliusoma na kuuelewa vyema mwanangu akiwa na wiki moja tu. Nikashauriana na mkr wangu kuwa mtoto tusimlaze tena kwa tumbo.
Baadae mwanetu akaanza kusimbuliwa na tumbo kujaa gesi, tukaambiwa eti ni kwa sababu ya namna tunavyomlaza. Je kuna uhusiano wowote kati ya mtoto anavyolala na tumbo kujaa gesi?

Ninavyofahamu mimi ni kwamba swala la mtoto kujaa tumbo ni kutokana na kutocheulishwa baada ya kunyonya au baada ya kulishwa. na hiyo hufanyika kwa mama kumbeba mtoto kwa kumlaza begani huku akimsungua mgongoni taratibu mpaka acheue ndipo amlaze kitandani chali.....
 
Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
0
Ninavyofahamu mimi ni kwamba swala la mtoto kujaa tumbo ni kutokana na kutocheulishwa baada ya kunyonya au baada ya kulishwa. na hiyo hufanyika kwa mama kumbeba mtoto kwa kumlaza begani huku akimsungua mgongoni taratibu mpaka acheue ndipo amlaze kitandani chali.....

Mtoto tunamcheulisha sana, na sasa tumeamua kutumia dawa inaitwa 'infacol'
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
1,000
Mtambuzi In short, kuna sababu nyiiingi ambazo zinaweza kusababisha SIDS, lakini ndio hivyo ni vigumu kutambua ni nini hasa kinachosababisha mtoto kufariki ghafla. Unaweza kufuata ushauri woote wa wataalamu na mtoto akafariki na madaktari wakashindwa ku pin point ni nini hasa kilichosababisha kifo cha mtoto. It's unfortunate and nothing to do with witchcraft. Hicho ni kisingizio tu cha kupata closure baada ya kifo cha mtoto.
 
Last edited by a moderator:

Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,461
2,000
duh hii kali, ndo naisikia leo.....
@ciello mpendwa jana saa kumi tumemzika mtto wa miezi 4 yaani ukikaangalia hako katoto utalia machozi nilishtuka sana emelda was very young ,na imetokea tu kama Mtambuzi anavyo dadavua juzi ijumaa alianza tu kulia lia then ikafika jmosi wakampeleka hospitali kufika wanataka kutoa damu wampime haikutoka damu kabisa hata tone na haikuchukua muda akafia singizini.it was so sad to me jamani the way i love kids nimeumia sana acheni tu jamani.hii inapaswa kuzingatiwa kama wenzetu walivyoweza kulitokomeza tatizo hilo kwa asilimia kubwa .
na pia Mtambuzi watoto wa chini ya umri wa mwaka wanahitaji uangalizi mkubwa tena wa mara kwa mara maana waompaka ugonjwa ufike kritical ndio utagundua so unahitaji kumenvestigate mara kwa mara.

Last edited by a moderator:

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
2,000
Asante sana Mtambuzi kwa elimu ya bure lakini yenye thamani.
Lakini nina maoni yafuatayo kwako
::
Kama alivyokuwa Munga Tehanan na gazeti la JITAMBUE unaonaje ukitafuta wasomi wengine wenye mwelekeo kama wako ili muombe ufadhili mtoe gazeti lenye mtazamo kama wa Jitambue?
::
Maarifa yako ni lulu inayohitajika sana lakini ni adimu kama Kakakuona,je huoni kuwa ni busara sasa Kuanzisha darasa special lessons in series hapa hapa Jf MMU,ikiwa ni upendeleo maalum wa maarifa yako kwa wana Jf,,

Nimekusikia mkuu, ngoja nilifanyie kazi, kuhusu hilo la special lesson, mbona darasa hilo lipo hapa MMU na wenzako wananufaika nalo, labda kama hufuatilii mada zangu humu JF
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom