Vifo vya watoto usingizini: Uchawi au ujinga…?

Nicas Mtei

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,564
1,250
sijawahi kutoka kapa kila nisomapo mabandiko y Mtambuzi.... nimejifunza mengi sana
 
Last edited by a moderator:
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,035
1,500
Dah, hadi niiformat brain yangu niamini chali ni salama kwa mtoto si leo.

Sie tulikuwa tunafundishwa kumlaza mtoto kifudi fudi, afu kichwa kinatazama pembeni, kwa usalama wake.
Kuna watoto ambao hucheua wakiwa usingizini, kama kalala chali uwezekano wa kupaliwa ni mkubwa, ila kama kalala kifudifudi mcheo hutoka.

Anyway, kama utamlaza mtoto chali, basi hakikia umemcheulisha baada ya kunyonya.

Ila kwa mie, mtoto halali mbali na mie, eti nimemlaza chumba cha nane mie niko sebuleni, hapana kama nina kazi bora nimbebe mgongoni niendelee na shughuli zangu.

Mtoto mtamu jamani.
Mtambuzi, nakubaliana na wewe kabisa. Watoto wengi wanasumbuliwa na lishe duni, mie hata 'kubemenda' nakuhusisha na kwashiorkor ama marasmus

Afu wamama wabishi tu, ila mtoto akinyonyeshwa maziwa ya mama bila kula kitu kingine kwa miezi 6 ya mwanzo, angalau basi minne haugui na afya yake inaimarika mno.
 
Jiwe Linaloishi

Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
May 24, 2008
3,736
1,225
Nakubaliana na wewe mkuu, na mtu kama Dr. Riwa anahusika sana.............
kweli mkuu ni vizuri kuwe na elimu angalau kuanzia shule msingi ili vijana wetu wakue wakiwa na upeo mkubwa kuhusu jambo hili.
hakuna vitu vinavyosikitisha kama vifo vya mama na watoto, hebu fikiria mke akiwa mjamzito tunavyofurahia na kuwa na matarajio kibao ghafla yanatokea mambo yanaweza kuzuilika yanamchukua.
 
Nyati

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,283
2,000
Mtoto tunamcheulisha sana, na sasa tumeamua kutumia dawa inaitwa 'infacol'
Mimi nilishauriwa na Dr. pale Morocco kwa Massawe lkn siyo Masawe ni mwingine ana jina la kiislamu, kuwa hiyo ni mbaya kwani inaathiri IQ ya mtoto kasema nisimpe. alishauri mama yake amnyonyeshe akiwa amekaa na akaaonyesha jinsi ya kumshika mtoto( hivyo mtembelee, si rahisi kuonyesha hapa), pia akashauri kuakikisha mtoto anacheua baada ya kunyonya, alishauri mimi (baba yake) nimbebe kifuania kwani kipo flat, baada ya haya tatizo lilipungua
 
piper

piper

JF-Expert Member
Jan 17, 2012
3,254
1,195
Ama kweli watoto wengi hupoteza maisha kwa kutojua kwa wazazi
 
I

IRINA

Member
Oct 24, 2012
23
0
Samahani chali na kifudifudi ina tofauti gani?
Chali ni kulala kwa kutumia sehemu ya nyuma ya mwili i.e kulalia mgongo wakati kifudifudi ni kujilaza kwakutumia sehemu ya mbele ya mwili yaani unalalia tumbo ,na ndio maana ni rahisi kwa mtoto kuishiwa hewa haswa hao ambao hawawezi kujigeuza maana wawezakaweka uso kiupande lkn katika kuhangaika ndo hivyo tena anawezalalaia hata uso ambao unainlude pua
 
T

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,520
1,195
darasa lako nafuatilia sana ila kusudio langu lilikuwa unapokuwa na mada fulani mf.malezi ya watoto basi unaichambua nje ndani kwa sehemu ya 1 2 3 4 5 n.k hata ukiandika toleo lijalo basi Tufatilie.OTHERWISE THANKS FOR NICE JOB
 
kalou

kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,908
2,000
Miezi mitatu nyuma dada yangu alifiwa na mtoto wake wa kiume(chini ya mwaka 1) akiwa usingizini..haya mambo mengine itabidi nimtafute ili nimpe elimu niliyoipata hapa
 
Fixed Point

Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,312
1,225
Dah, hadi niiformat brain yangu niamini chali ni salama kwa mtoto si leo.

Sie tulikuwa tunafundishwa kumlanza mtoto kifudi fudi, afu kichwa kinalazama pembeni, kwa usalama wake.
Kuna watoto ambao hucheua wakiwa usingizini, kama kalala chai uwezekano wa kupaliwa ni mkubwa, ila kama kalaa kifudifudi mcheo hutoka.

Anyway, kama utamlaza mtoto chali, basi hakikia umemcheulisha baada ya kunyonya.

Ila kwa mie, mtoto halali mbali na mie, eti nimemlaza chumba cha nane mie niko sebuleni, hapana kama nina kazi bora nimbebe mgongoni niendelee na shughuli zangu.

Mtoto mtamu jamani.
Mtambuzi, nakubaliana na wewe kabisa. Watoto wengi wanasumbuliwa na lishe duni, mie hata 'kubemenda' nakuhusisha na kwashiorkor ama marasmus

Afu wamama wabishi tu, ila mtoto akinyonyeshwa maziwa ya mama bila kula kitu kingine kwa miezi 6 ya mwanzo, angalau basi minne haugui na afya yake inaimarika mno.
hata mimi ndo naisikia leo kuwa ulalaji wa chali ni salama pia....
wanangu wote wamelala kifudifudi mpaka wamekuwa wakubwa sasa wanajipindua wenyewe.
mimi mwenyewe sipati usingizi nisipolala kifudifudi, lol! na naambiwa tangu nilipofundishwa kulala kifudifudi nilipozaliwa.
kumcheulisha mtoto baada ya kunyonya ni muhimu sana lakini wakati mwingine gesi haitoki ikaisha, ukimlaza kifudifudi na kama bado ana gesi utaisikia ikitoka, akilala chali inaishia wapi? sijui
 
nyumba kubwa

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,314
2,000
Mimi mwenyewe ni naamini kwenye kumlaza mtoto kifudi fudi...na wanasema ukiona mtoto amepata nguvu za kuinua kichwa jua hawezi kulalia pua atafurukuta alale sawa. Ila nachojia mito na mazaga zaga mengine ni hatari sana kitandani kwa mtoto....mito inaua sana.

Nilishawahi sikia inshu moja majuu mtoto alijiziba na mto wakati baba, mama na auntie yake wanapiga story sebuleni chini mtoto kalala chumbani ghorofani, akawa wa blue wamemfikisha hospital (na helikopta) kakutwa brain imeshaharibika...akaendelea kupumulia mashine;moyo huko safi brain haifanyi kazi kabisa....mwisho wa siku wazazi wa kale katoto wakaamua ku donate moyo wa mtoto wao kwa familia yenye mtoto same age iliyokuwa inatafuta donor wa moyo...na wanasema wamefarijika kujua moyo wa marehemu mtoto wao unahishi kwa mtoto mwingine na wamemfanya huyo mtoto part ya familia yao.
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,035
1,500
itabidi Mtambuzi utueleweshe vizuri zaidi, kumbe siko peke yangu nayeamini kulaza kifudifudi.

Umewasikia FP na nyumba kubwa pia.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
itabidi Mtambuzi utueleweshe vizuri zaidi, kumbe siko peke yangu nayeamini kulaza kifudifudi.

Umewasikia FP na nyumba kubwa pia.
Kumlaza mtoto kifudifudi sio kwamba ndiyo sababu pekee inayosababisha vifo hivyo, mbona nimetaja sababu nyingi tu, mbona mmeshupalia hiyo ya kulala kifudifudi...!

Iko hivi, nimeeleza kwamba kumlaza mtoto kifudifudi kwenye blangeti la sufi au mto laini ndio husababisha madhara kitu ambacho hata nyumba kubwa amekubaliana na hoja yangu.

kwa kule marekani matumizi ya ma blangeti ya sufi laini ni makubwa kutokana na hali ya hewa tofauti na Dar, hivyo hoja hiyo inaweza ikawa haina mashiko kwa mkazi wa Dar, lakini ikawa na mashiko kwa mtu wa Mbeya au Mafinga Iringa.

Soma tena nilichoandika........

na ukipata muda pitia hizi link hapa chini:

Safe to Sleep Public Education Campaign

Tummy time - Wikipedia, the free encyclopedia

Back to Sleep campaign urges careful care of infants | Deseret News
 
Last edited by a moderator:
cacico

cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,377
1,250
jamani kama mtoto unamtaka, mimba ikiharibika hata wa wiki 1, roho inauma sana! nilipata two miscarriages za miezi mi3 na mi4! nikuwa nalia kama nimefiwa mtoto kabisaaaaaaa, yaani ndugu zangu walikuwa wanapata kazi ya ziada kunibembeleza!! ndio MUNGU akanizawadia twins baada ya hiyo misuko misuko!

kwa kweli kulea watoto chini ya mwaka mmoja ni ngumu, na inahitaji ulezi wa mama mwenyewe na si hausgal, kama mama yupo na ni mzima, jamani tujitahidi kulea wenyewe, hausgal awepo tu kama msaidizi, kufua, kuchemsha vyombo vya watoto etc! nilipopata twins, niliacha kazi!! for two years nimelea mwenyewe!! wanaanza baby class wana miaka mitatu, ndio na mimi nikarudi kazini!

hii ilinipunguzia kuuguza mara kwa mara! maana nasimamia kila kitu mwenyewe, neti ziwe safi, chupa zifungiwe kwenye container, no mbu wala inzi chumbani kwa watoto, maji ya kunywa ya watoto yachemshwe etc!!
kuhusu kulala watoto, kwakweli walipokata kitovu tu, niliwaanzisha kulala kifudifudi, ila nahakikisha hakuna nguo yoyote pembeni, namlaza juu ya godoro bila shuka, vile vigodoro vya watoto, mpaka walipozoea nadhani mwaka mmoja na nusu, ndio nikaanza kutandika mashuka! ila ukimlaza kifudifudi analala zaidi kuliko ukimlaza chali!!

MUNGU WETU AWALINDE WATOTO WETU WAKUE, WATUZIKE! Amen!
 
Karucee

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
14,481

amen darling. A big Amen na pole kwa misukosuko ulopata. You have really inspired me.
 
M

magegeg

New Member
Dec 6, 2012
1
0
:A S angry: tumekupata sana mjomba, zingatia maswali mengine yasiyo na msingi.!
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,412
2,000
amen darling. A big Amen na pole kwa misukosuko ulopata. You have really inspired me.
hivi dada yangu una mtoto? Maana dah, nahisi kama ni wa kiume chekechea ataua wenzake, loh!
 
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,178
2,000
somo zuri sana hili Mtambuzi, thanks
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,026
2,000
Unayoyasema kuhusu hali duni ya uchumi na makazi duni kusababisha vifo vya aina hiyo nakubaliana na wewe.
Nakumbuka miaka ya 80 wakati naisha Mwananyamala vifo vya wa watoto wachanga vilikuwa vinatokea sana na watu walikuwa wanashikana uchawi ile mbaya.

Baada ya kusoma huo utafiti ndio nikagundua kwamba ule ulikuwa ni ujinga tu. Kunahitajika elimu hii itolewe wakati kina mama wanapohudhuria kliniki............
Nimesoma na nimeguswa sana! Mwaka huu mwanangu alifariki mara tu baada ya kuzaliwa na mama yake hakuiona hata maiti ya mtoto wake! Hapa nilipo machozi yananilengalenga!
 
Mtotowamama

Mtotowamama

Member
Oct 25, 2012
61
95
Nashukuru kwa darasa zuri na ambalo linanihusu. Mbarikiwe nyote mliotoa elimu hii kwetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom