Wingawinga
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 621
- 1,524
- Thread starter
- #261
Ebana ume nikumbusa kitu, ngoja nikupe hii sad story halafu ndio nije ni kuchane kwa wivu wako ka watoto wa kishua .Makatta nilikuwaga nasoma tangazo la familia gazeti la Uhuru wkt wa kuadhimisha siku ya kifo chake. Walikuwa wanaweka hadi picha enzi hizo. Sasa wivu wa kuishi Oysterbay ndiyo visababishe kijana kurushwa kutoka ghorofani? Hizo siyo sababu zenye ushawishi au nguvu za kutosha za kufanya mauaji ya kinyama kama hayo.
Baada ya Makatta kuwawa, tulikuwa na famili friends zetu hao walikua wanakaa mtaa wa Ethiopian cresent and Winding , kwenye hiyo familia Baba yao alisha fariki ( tena naye Kifo cha kutatanisha tetesi alikuwaga judge or hakimu sikumbuki vizuri ). katika hiyo familia kuna mabinti kama 4 na mvulana mmoja.
Suku Makatta amefariki ndio ikabidi kuweka tangazo la kifo kwnye radio na gazeti, Sasa siku nime kaa nyumbani, akaja mmoja wa hao sisters akaniuliza ,kuna gazeti la leo ? nikamjibu ndio , akaniambia wametoa tangazo la Makatta naomba niletee nione, nikaingia ndani nika mletea , kipindi hcho sikumbuki kama nina jua kusoma au la , basi akaaza lisoma kwa sauti na ninakumbuka aksomasehemu ya hilo tangazo ikisema "Baada ya kuwawa kikatili ghorofani" .
Kinacho sikitisha ni kwamba bila kujua ni kwamba naye baada ya muda dada yake anakuja uwawa kwa kurushwa ghorofani wao nao wakatangaza kwenye gazeti hivyo hivyo kusema "Baada ya kuuwawa kikatili ghorofani " ,yeye aliitwa Adelide dada yake aliye uwawa aliitwa Angelica , nadhani kama ulisoma tangazo la makatta utakumbuka kwamba kuna sehemu ilisema "baada ya kuwawa kikatili ghorofani "