Vifo vya Magufuli na Ndugai vimetoa funzo kwa watanzania

Vifo vya Magufuli na Ndugai vimetoa funzo kwa watanzania

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,832
Reaction score
25,138
Neno la Mungu linasema kwamba ukimtendea mwenzako ubaya utalipwa hapa hapa duniani. Huu ni ukweli wa wazi na ambao huwezi kuukwepa kwa kuwa umefungamanishwa na neno la Mungu.

Mwaka 2017 mheshimwa ndugu Tundu Antipas Mugway Lissu alinusurika kuuawa na watu wasiojulikana mchana kweupe mbele ya makazi yenye walinzi na CCTV cameras 24/7. Kila mtanzania mwenye akili anajua nini kilichojiri isipokuwa wale wapumbavu wachache wanaopenda kujitoa akili. Watu wote walibaki wanajiuliza: Wanapomuua TAL hivi hawajui kuwa huyu ni baba na ana watoto, mke na ndugu wanaomtegemea? Je, aliwakosea nini hadi kutaka kumtoa roho yake kikatili namna ile? Kama hawampendi si afadhali wangemtilia sumu kwenye chakula afe taratibu kama walivyomtilia sumu Philip Mangula na Harrison Mwakyembe?

Baada ya Tundu Lissu kupelekwa kwenye matibabu huko Nairobi na hatimaye Ubelgiji, Job Ndugai akamfuta ubunge na akagoma kuidhinisha gharama matibabu kama ilivyo kawaida kwa wabunge wote wanaotubiwa ndani na nje ya nchi. Pamoja na kufutwa ubunge pia waligoma kumlipa mafao yake ya ubunge na hata Samia alipoapishwa kuwa Rais hajawahi kumlipa hata senti moja ya malimbikizo ya mishahara yake wala posho ya ubunge.

Licha ya TAL kupitia madhira yote haya, wamembambika tena kesi ya uhaini na kumfungia gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Mpaka naingia mitamboni, TL bado anahangaika gereza la Ukongo licha ya majeraha ya risasi zilizonusurika kumuua pamoja na vyuma alivyofungwa mwili mzima baada ya kuchakazwa na risasi za watu wasiojulikana.

John Magufuli, aliyekuwa Rais wakati TAL anauliwa kwa risasi lakini hakuchukua hatua yoyote ile, amelala mavumbini. Amewaacha wake zake na watoto (Janeth na wadogo zake wengine). Job Ndugai, aliyemfuta ubunge TAL na kumyima pesa za matibabu na mafao, naye anaoza kaburini. Wake na watoto ambao Magufuli na Ndugai wamewaacha hapa duniani, licha ya kulipwa na serikali 80% ya mishahara waliyokuwa wakilipwa waume zao (kama wenza wa rais na spika), wamebaki yatima na wapweke.

Wakati huhuo, TAL aliyefanyiwa vituko vyote hivi, bado yuko hai anaendelea kuvuta pumzi. Kwa mfuatano huu wa matukio ya malipo yanayofanyika kwa watesi wa TAL, tusishangae hata mtu anayemtesa gerezani naye akafuata njia hii hii. Mungu hadhihakiwi na wala hawajawahi kushindwa kuwatetea waja zake. Stay tuned and alert. Anything can happen in the near future.
 
Screenshot_20251201-222021~2.png
 
Lissu alishawahi kutamka hadharani kuwa kalipwa stahiki zake na Rais Samia. Kuhusu vifo ni kuwa kila mtu atakufa.. kuna watu wema wengi wamekufa na waovu kibao wanadunda. Hakuna somo lolote kwenye kifo. Ingekuwa kifo ni adhabu basi mtu kama Alex Massawe (AM) dhulumati la kimataifa angeshaondoka kitambo sana.
 
Masawe kaishia kusilimu,sasa hivi alhajj swala tano,akifa anaenda kuchakata mbususu na mitungi
 
Lissu alishawahi kutamka hadharani kuwa kalipwa stahiki zake na Rais Samia. Kuhusu vifo ni kuwa kila mtu atakufa.. kuna watu wema wengi wamekufa na waovu kibao wanadunda. Hakuna somo lolote kwenye kifo. Ingekuwa kifo ni adhabu basi mtu kama Alex Massawe (AM) dhulumati la kimataifa angeshaondoka kitambo sana.
Mungu ni ufundi. Anajua muda sahihi wa kuchukua hatua
 
Nilifufahi sana siku ile
Siku lisu anapigwa risasi au siku kigogo anatangaza tweeter kuwa magu hayupo tena na akasema picha ya gari la kubebea maiti lenye mzinga nyuma likikatiza mitaa ya dar?
 
Wengi wamesema. Ni suala la muda tu.

Kuna mtibeli humu alishaonya lkn wamekaza shingo.
 
Back
Top Bottom