Ambiente Guru
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 2,623
- 1,096
Imethibitishwa kuwa rubani mdogo wa ndege Ufaransa aliingilia mitambo kwa makusudi na kuangusha ndege milima ya Alps wiki hii.
Kabla alimfungia nje rubani mkuu na kuishusha na kugonga ndege hiyo milinani.
CHANZO: BBC
Kabla alimfungia nje rubani mkuu na kuishusha na kugonga ndege hiyo milinani.
Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo alikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.![]()
Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''
''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''.
CHANZO: BBC