Vifaa vya kijasusi vya kisovieti vilivyotumiwa kipindi cha vita baridi vyapigwa mnada

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,617
32,723
Vifaa vilivyotumiwa na majasusi wa Umoja wa Kisovieti katika vita baridi hivi karibuni vyanadiwa.

Kikundi cha urithi wa vita baridi ikiwemo silaha za siri za Umoja wa Kisovieti hivi karibuni kimenadiwa kwa paundi laki 3.65 za kiingereza.

Vitu hivi mia nne vilihifadhiwa na mkusanyaji kutoka Ulaya katika miaka 30 iliyopita, ambaye alifungua jumba la makumbusho la kamati ya usalama wa taifa ya kisovieti ya KGB mwaka 2019 huko New York.

Lakini jumba hilo lililazimishwa kufungwa kutokana na mlipuko wa COVID-19, na mkusanyaji huyo amenadi vitu hivyo alivyohifadhi.

Picha 1: Tai yenye kamera za siri inayouzwa kwa paundi 2,200 za kiingereza

Picha 2: Bunduki ya kalamu ya kijasusi ya KGB

Picha 3: Mwavuli wa kijasusi wa KGB wenye sindano ya sumu

FB_IMG_16150959346278728.jpg
FB_IMG_16150959314351508.jpg
FB_IMG_16150959277276592.jpg
 
Hata hapa kwetu miaka ya nyuma kulikuwa na pen, saa au pete zote zenye kamera za kijasusi. Msiulize ulijuaje.

Nahisi hata leo wale wa suti nyeusi hivyo vitu bado wanavitumia.
 
Miaka hiyo kumbe jamaa wana hadi camera ndogo za kwenye tai
Mkuu hapo ndo utakapoamini haya mapengo hayatakaa yazibike kwa nchi zetu zinazoendelea.

Huo umoja wa kisovieti majaribio ya makombora ya kati na masafa yalikuwa kawaida tu.

Ilifika hatua mpaka Marekani mwenyewe aliogopa. Mwisho wakaona bora hizo tofauti za vita baridi wazimalize. Usalama wa dunia ulikuwa kwenye tishio kutokana na hiyo vita baridi.
 
Miaka hiyo kumbe jamaa wana hadi camera ndogo za kwenye tai
Teknolojia tunayoitumia watu wa kawaida muda huu, mashirika ya kijasusi kwenye mataifa makubwa kama Uingereza na Marekani, waliwahi kuitumia kuanzia miaka ya mwishoni mwa 1950's. Walichokuwa wana miss kwa wakati huo ni mobile phones tu, lakini kila kitu tunachotumia watu wa kawaida kwa muda huu, walikuwa nacho na walikuwa wanakitumia. Kwa sasa hivi, wao wanaweza kuwa wanatumia teknolojia ambayo sisi tunaweza kuja kuitumia kama miaka 30 au 40 ijayo, wao wakati huo wakiwa wameshaiacha siku nyingi.
 
Hata hapa kwetu miaka ya nyuma kulikuwa na pen, saa au pete zote zenye kamera za kijasusi. Msiulize ulijuaje.

Nahisi hata leo wale wa suti nyeusi hivyo vitu bado wanavitumia.
Pen ninayo, usiulize nimepata wapi.
 
Back
Top Bottom