Viettel Wamekuita kwenye Interview?

Viettel Wamekuita kwenye Interview?

Mangi wa Rombo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
202
Reaction score
138
Habari wana JF!
Kuna hii kampuni ya Viettel ilitanganaza nafasi za kazi nyingi tu! Mimi nilijaza nafasi hizo! Leo nimepokea email kutoka kwao "viettelrecruitment" ikinitaarifu kuwa wata-conduct interview tar 6/10 hivyo nithibitishe kama nitahudhuria! Swali langu ni, je kuna mtu mwingine yeyote humu ndani amewahi kuitwa? Na kama yupo ni test gani walizokupa kwenye hiyo interview?
Ahsante
 
achana nao.ni matapel tu hao.hakuna kampun inayoitwa viettel iliyosajiliwa kuoperate tanzania.endelea na shughul zako nyingine wala usiende kwenye hzo interview zao...kwan utakua unajipotezea muda wako bure
 
Last edited by a moderator:
Nenda kaongeze experience ya kuattend interviews kama upo Dar. Ila hii kampuni imeleta utata sana humu JF na ata wao VIETTEL TANZANIA hawajawa certified na Jamii Mods kwamba ni ID ya kampuni. Hawana web wala physical address wao wanadai ndio wana emerge so hivyo vitu bado. Ila nadhani tungekua tumeshaona sana matangazo ya.coming soon..

Pitia hii.link chini:
https://www.jamiiforums.com/nafasi-...a-utata-dhidi-ya-vietel-tanzania-company.html
Lol! Ahsante kwa msaada mkuu! Akili kumkichwa, wakitaka hela natokaje ndukiii!
 
Last edited by a moderator:
Lol! Ahsante kwa msaada mkuu! Akili kumkichwa, wakitaka hela natokaje ndukiii!

hawatataka hela yako ata sent kwenye process nzima ya usaili.ila narudia tena viettel tanzania ni matapeli na wahuni.usipoteze muda wako kuapply wala kwenda kwenye interview.kama kuna mtu ana swali lolote kuhusu viettel tanzania na auniulize hapa.maswali yote yatajibiwa.nimefanya uchunguzi wa zaid ya miez sita kuhusu hawa watu na sasa naweza sema kwamba nina hard facts na evidence zizopingika bila mashaka yoyote kuwa hawa watu wanaojiita ni viettel tanzania ni wahuni na matapeli wakubwa
 
Nenda kaongeze experience ya kuattend interviews kama upo Dar. Ila hii kampuni imeleta utata sana humu JF na ata wao VIETTEL TANZANIA hawajawa certified na Jamii Mods kwamba ni ID ya kampuni. Hawana web wala physical address wao wanadai ndio wana emerge so hivyo vitu bado. Ila nadhani tungekua tumeshaona sana matangazo ya.coming soon..

Pitia hii.link chini:
https://www.jamiiforums.com/nafasi-...a-utata-dhidi-ya-vietel-tanzania-company.html

Usiongee kitu ambacho huna uhakika nacho. Nyie mnadhani kufungua kampuni ya simu ni sawa na kufungua mgahawa. Usiwakatishe tamaa watu. Hao Viettel wapo sana tu, sasa wanapatikana GEPF tower. Website yao official ni www.viettel.com.vn/Map.html. Mnadanganywa na huyo jamaa Don Mangi aliyejifanya kuwajua Viettel kama matapeli, kumbe yeye ndio mwongo.
 
wewe hata hujui unachokiongea.na ni bora ungekaa kimya.au na we ni mmoja wao hawa 'vietel tanzania'? kaka nina uhakika 100% hakuna kampuni inayoitwa VIETTEL TANZANIA.nenda brela ambaye ndo msajili wa makumpun hapa tanzania.hawa jamaa hawapo.nenda tcra ambayo ndio hutoa lesen kwa telecom and mobile operators hawa jamaa hawapo pia. ukitaka nifunguke ntafunguka zaid ya hapa. ila kwa kifup hawa jamaa ni matapel
 
Last edited by a moderator:
1.vietel tanzania haijasajiliwa kama kampun tanzania.
2.viettel tanzania haitambuliki na TRA wala haina TIN number.
3.viettel tanzania haitambuliki na tcra
4.viettel tanzania haijawah kutoa tangazo lolote lile la kazi au tenda katika gazeti lolote lile linaloaminika ndan au nje ya nchi zaid ya hivi vioja tunavyoviona vya kuapply kupitia email ya gmail
 
Brela brela. Usikariri wewe. Unajua maana ya Brela wewe? Unaambiwa kampuni ipo. Jaribu kujishughulisha hata kusoma machapisho kwenye mtandao. Viettel wamenunua leseni kwa watu gani kwanza? Wenzako washapelekwa mikoani wewe wasema brela brela. Nenda GEPF tower kawaulize hao Viettel kwanini hawako huko Brela kwako.
 
uspanick mkuu.uatelewa tu.ila kabla hatujaenda mbal nikuulize labda wewe una mahusiano gan au maslah gan binafsi na hawa wavietnam
 
1.vietel tanzania haijasajiliwa kama kampun tanzania.
2.viettel tanzania haitambuliki na TRA wala haina TIN number.
3.viettel tanzania haitambuliki na tcra
4.viettel tanzania haijawah kutoa tangazo lolote lile la kazi au tenda katika gazeti lolote lile linaloaminika ndan au nje ya nchi zaid ya hivi vioja tunavyoviona vya kuapply kupitia email ya gmail

Kaka usije ukaibiwa kwa sababu ya kuamini private emails. Kampuni ya mdogo wangu ni ndogo sana lakini inatumia private emails. private email kwa mwaka haigharimu zaidi ya dola 60. Mtu yeyote anaweza kufungua. Emails zangu pia ni private, lakini hii haioneshi kwamba mimi ni mtu wa kuaminika.
Watu hupenda kutumia gmail kwa sababu nyingi. Size utakayopata gmail inaweza ikawa kubwa lakini pia hawaiweki email email yao katika risk ya spams, na pia kuingiliwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni.
Hayo mambo mengine ya TIN na TRA nadhani mnajifanya mwajua wakati hamjui. Umeenda mara ngapi kuomba TIN number ya mwajiri unapoenda kuomba kazi? Mfano unaenda kuomba kazi IPP, je utaanza kuuliza TIN number. Kampuni ngapi za Tanzania unajua zina TIN number. Nadhani hapo utakuwa mwehu tu.
 
uspanick mkuu.uatelewa tu.ila kabla hatujaenda mbal nikuulize labda wewe una mahusiano gan au maslah gan binafsi na hawa wavietnam

Nina kazi kubwa tu yangu binafsi tena ya halali. Siwezi paniki kwa ujinga wa watu wanaodhani wanajua kumbe hawajui. Ila napata hasira kuona mtu asiyejua anajifanya anajua. Lakini usitake kudanganya watu kwa kitu usichokijua ukijifanya unajua. Shemeji yangu tu alipata kazi hapo Viettel lakini bahati nzuri kaitwa TPDC. Nilishawahi waambia watu mimi namjua hadi Mvietnam human resource manager. Lakini pia nilishawaambia watu kwamba wasitegemee kulipwa mishahara mikubwa... Kama mtu haamini si aende GEPF Tower aulizie office za Viettel na kuongea nao?
 
kaka usipende sana kwenda nje ya mada.kila mtu ana kazi yake pia tena ya halali.tusianze kulingishiana huyu ana nini au huyu hana nini kwan hayo ni mambo ambayo yako irrelevant ukicompare na topic tunayoijadili.pia nashukuru kuwa kumbe wewe si mmoja wao.mimi pia inaniuma sana ninapoona vijana tena graduates wanaporubuniwa na hawa matapeli wanaotaka kunyonya nguvukazi za graduates kwa mgongo wa foreign investment.sasa naomba step by step tuanze kulidadavua hili suala kwa manuafaa ya wote.sina nia mbaya na na naamin wewe pia huna nia mbaya.na hii ni kwa manufaa ya wote.
epocha and golden oceaan tanzania limited yenye ofisi zake NHC house biashara complex floor ya pili mwananyamala, mwinjuma road. ilianzishwa na kusajiliwa BRELA kama kampun tar 3.6.2005 na bwana abdalah mnende.mwaka 2008 ilifanikiwa kupata national and international network facility (NF) licence ya kuoperate kama mobile and telecommunications company kutoka tcra kwa gharama ya sh za madafu bilion 1.4. hii ni gharama ya lesen peke yake.iliplan kulaunch operations zake kama cellular telecomunications company na mobile operator nchi nzima kwa proposal buget ya 200 milion usd mnamo januar 2011 lakin ikashindkana obvisiouly kwakua hawakua na kias hicho cha pesa. mnano sept 2012 viettel global investment group ilinunua 65% ya share za epocha and golden ocean tanzania ltd almaarufu kama EGOTEL(epocha and golden ocean tanzania limited) kwa gharama ndogo tu ya usd 18 million. hapo ndipo wavietnam walipofanikiwa kuingia tanzania.................nitarud baadae na documented evidence kukuthibitishia mkuu ozzie kwa nini nasema viettel tanzania ni kampun ya kitapeli
 
Kwa wakazi wa Mbeya leo ndio interview na ujumbe waliotumiwa uko hivi, angalia lugha iliyotumika:.......

Viettel Tanzania Company notify. 13:00Pm-Tomorow(04-october-2014), You come my office to recruitment exam. Add office: veta street, plot no 146, block D, ilomba area - mbeya municipal. Call help: Vitalis 0766.758.450
 
wewe hata hujui unachokiongea.na ni bora ungekaa kimya.au na we ni mmoja wao hawa 'vietel tanzania'? kaka nina uhakika 100% hakuna kampuni inayoitwa VIETTEL TANZANIA.nenda brela ambaye ndo msajili wa makumpun hapa tanzania.hawa jamaa hawapo.nenda tcra ambayo ndio hutoa lesen kwa telecom and mobile operators hawa jamaa hawapo pia. ukitaka nifunguke ntafunguka zaid ya hapa. ila kwa kifup hawa jamaa ni matapel

Hiyo kampuni ipo ninauhakika, jamaa yangu aliomba akajaza ile form alishafanya interview na sahivi yupo kazini tokea tarehe 22/9, mimi binafsi nilipuuzia kuijaza kwa mtazamo kama huo, kingine kuna jina la kampuni na jina la biashara nadhani jamaa anatafuta VIETTEL TANZANIA huwezi ikuta ni sawa na kutafuta TIGO TANZANIA huwezi kuta, upande wa tigo ukienda brela, TCRA, utakuta wanaitwa MIC TANZANIA.
 
baada ya kuingia tanzania mnamo mwaka 2012 chini ya mgongo wa epocha and golden oceanic tanzania limited(egotel) ambayo ilikua kampun ya mzawa bwana abdalah mnende. vietel ilianza hila na ujanja.viettel global investment group wakaanzisha kampun hewa ya simu na kuiipa jina 'viettel tanzania company' narudia tena kampuni hili halijasajiliwa popote pale si BRELA si TRA si TCRA.hili si jina la biashara na wala si kampun kwan halijasajiliwa katika mamlaka yoyote hapa nchini na kisheria ni makosa kutumia neno 'company' kwa shughuli zozote ziwe za usaili au biashara bila kufanya usbrela. walianza kwa keo pale sophia house migombani street plot no 145 mikocheni baadae wakaamia gepf house floor ya pili karibu na victoria ali hassan mwinyi road ambapo wapo hadi leo.uhuni wa hawa wavietnam ni kwamba
1.wanaadertise kazi kwa jina la kampun ambalo halipo 'vietel tanzania company' badala ya kuwaambia ukwel watu kwamba kampun wanaloenda kulifanyia kaz ni epocha and golden ocean tanzania ltd'egotel'
2.kazi wanazotangaza ni tofauti na kazi ambazo wanawapa waajiriwa.kwa mfano graduate wa telecom anaaply kama teleom staff mwisho wa siku anapewa kazi ya ukariman na tour guide ambapo analazimishwa kuwa msaidiz, mbeba mizigo na mtafsir endapo hawa wavietnam watahitaj kuwasiliana na wazawa ukizingatia kwamba hawa wavietnam hawajui kiswahil wala kiingereza.trust me hawajui kabisa kiingereza.hivyo wanaitaj watafsir sasa bila aibu wanawageuza wasomi maeengineer wetu kuwa wakarim3.vietel tanzania ndio kampun pekee dunian inayotoa flat rate ya msharaha, sio mshahara kwa maana ya salary bali ni wages za Sh 400,000 (kwa wale msioelewa jaribun kugoogle ili mjue tofauti kat ya salary na wages) vietel tanzania wanawalipa wafanyakaz wao wages na sio salaries(refer kwenye attachment ya mkataba wao hapo chin) hivyo basi kabla ya makato kwa watu wa engineering, computer science, bcom,bussiness administration, b.arts, madereva, marecptionists, watu wa human resource, etc. .........wote hawa wanalipwa lak nne kamil kabla ya makato.kwa scale za tra za pay as yo earn(paye) tax ni 20% ambayo ni elf 80 katvya lak 4 kamil.ukijumlisha na mifuko ya kijamii kama nssf au ppf 10%.take home ya waajiliwa wote wa 'vietel tanzania' ni sh 280,000 kwa mwez.
4.viettel tanzania ni wapumbav, waongo naanyonyaj wa kutupwa. wamewaambia wafanyakaz wao wapya wajigharamikie naul na malaz ya kwenda mikoan bila allowance, bila transport costs, bila gharama za kujikimu kabla ya kupewa mshahara wa kwanza, wala bila per diem kwa ujira wa lak 280 kwa mwez.kwel hii ni halal?ata mwalimu wa shule ya msing ana unafuu........
5.vietel tanzania inatumia jina la egotel inapoingia mikataba na waajiriwa wake.mkataba unaandikwa agreement between 'egotel' as an employer and ...... as an employee. kwanini kwenye mikataba yao ya kazi wanatumia jina la epocha..(egotel) wakat kwenye kuapply nafas za kaz na kuajiri wanawaambia watu mnaajiriwa na kampun ya vietel tanzania?
6. mikataba ya ajira na ya kukodisha maeneo ya kujenga minara mpangishaji na mwajiri ni epocha...(egotel) neno vietel tanzania linatoka wap? ninayo mikataba yote ya kupangisha maeneo kwa ajiri ya kujenga minara na yote nitaiweka online ili watanzania wote waione.
7.kama kampun ni egotel kwanini mnadanganya watu kwamba wameajiriwa vietel tanzania? na kwa nini hawaheshimu profession za watu? utamlipaje engineer aliyesoma miaka nne chuo plus years of experience after school mshahara wa sh 280,000 kwa mwez bila allowance, bila accomodation, bila per diem ya aina yoyote tena kazi mkoan.
8.inakuaje contract of employment inakua haina job title na huwez amin kwa walio uliza waliambiwa eti job description unaambiwa utapewa ukifika kazin.hii imewakumba wale wote walioambiwa waende mikoan kuanzia majuz tu jumanne ya tareh 1.10.2014(ambao ndo intake ya kwanza) wameambiwa wakifika mikoan kwa gharama zao wenyewe ndo watapangiwa majukumu ya kazi.kama huu si uhun ni nini?
9.unawezaje kusign contract na mtu husiwe mjua na ambaye namba zake za simu na email yake inafichwa na ambaye hujawah kumwona eti anatwa.....na ndie managing director wa 'vietel tanzania'.ata copy ya contract hupew...kwel hii ni halal?.naapia hamna mwajiriwa wa vietel tanzania mwenye copy ya contract yake
10. ntarud tena. Kwa kifupi 'vietel tanzania company' haipo. Watanzania wenzagu kueni makini.hawa ni matapeli.hawana hela.ni waongo.wanastahil kuchukuliwa hatua au kufikishwa mahakaman kwa kurubun watanzania.nina meng ya kuongea.......ila inaniuma sana nikiona gratuates tena wa engineering na waajiriwa wengine wana masters,wanafanyishwa kaz za std seven leaver na mambo kama haya.......hawa jamaa ni wahun......nina document nyingine nying za kusupport haya ninayoyasema na zote nitazianika kwa uwazi hapa jf.
 
Attachments

  • IMG-20141001-WA0022.jpg
    IMG-20141001-WA0022.jpg
    107.8 KB · Views: 1,014
  • IMG-20141001-WA0023.jpg
    IMG-20141001-WA0023.jpg
    154.8 KB · Views: 924
  • IMG-20141001-WA0020.jpg
    IMG-20141001-WA0020.jpg
    190.2 KB · Views: 888
Aisee Mangi nikutoe shaka tu ni kwamba mimi pia niliwahi omba kazi kwa hawa jamaa miezi minne iliyopita na juzi nikatumiwa sms kunitaka nifike kwenye interview a dayvafter na kweli jana nifanya written interview hapa mkoani kwangu. So tusipende sana ku undermine watu kiasi hiki kama asemavyo Bw. Rearden, nradi wa hawa jammaa ni issue ndefu si kama unapotaka kufungua duka la samaki wabichi au grocery.
Nakushauri nenda kwenye interview upate uzoefu kwani interview zao ni nzuri sana na zote ni online na matokeo unayapata hapo hapo baada ya click finish.
 
Back
Top Bottom