Interview and employability; Usipozingatia haya, utaishia ku-apply kazi bila kuitwa kwenye interview

Sewando MP

Member
Jan 25, 2014
56
116
USIPOZINGATIA HAYA, UTAISHIA KU-APPLY KAZI BILA KUITWA KWENYE INTERVIEW

Vijana wengi sana Wahitimu wa vyuo wamejikuta katika janga la kuishia ku-apply kazi bila kuitwa kwenye Interview. Kwa miaka kadhaa nimekuwa kwenye Managerial Level katika taasisi ninazofanyia kazi. Na katika recruitments kashaa nilizozifanya kuajiri, nimekutana na changamoto nyingi sana kwenye applications za kazi zinazowafanya watu wengi kutokuwa shortlisted kuitwa kwenye Interview.

Tuko katika ulimwengu wa Utandawazi ambapo mfumo wa kuomba kazi Serikalini, Taasisi mbalimbali, na Sekta binafsi ni kwa njia ya Online (Online Job Application). Nimebaini Graduates wengi hawana Job Application & Employability Skills kuwawezesha kuwa shortlisted tu. Na shida kuwa nadhani ipo kwenye mfumo wetu wa Elimu ambapo hauendani na mahitaji ya sasa, kumfanya mtu ahitimu masomo akiwa na uwezo na maarifa flani ya ziada ya kumsaidia.

Sasa Leo, nitagusia vituvichache tu ambavyo watu wengi wamekuwa hawavizingatii pindi wanapoomba kazi Online. Kazi yoyote ile ambayo Application yake ni Online (kama vile kutuma kwa njia ya barua pepe), Interview ya kazi inaanzia;

1. How you arranged your CV
2. How you drafted your Application/Cover Letter
3. How do you send your Application

1. Application Letter - Application yoyote ya kazi, Application /Cover Letter ni muhimu, hata usipoambiwa utume. Labda kama itakuwa imeelekezwa vingine.

2. Unapotuma Application kwa njia ya Email (barua pepe)
(a). Letter Heading - Kwenye barua lazima utaje exactly position unayoomba kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi. Maana wakati mwingine Taasisi au kampuni hiyo wanaweza kuwa wametangaza nafasi za kazi za position tofauti tofauti.
(b). Kwenye Email Subject: You have to mention exactly the position unayoomba kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi na inatakiwa kuandikwa kwa herufi KUBWA - APPLICATION FOR CALL CENTER AGENT.
(c). Documents zako (CV & Letter) attachment zinatakiwa kuwa na Majina yako - Kongwa Dodoma Tanzania
(d).Kwenye email body, lazima uandike chochote, not just sending it plain. Mfano:

Hi Sir/Madam;

As per the subject, Kindly receive the attached CV and application later for your perusal/reference.

Thank You.

3. Kwa ujumla, wengi wanakosa kazi kwa kutozingatia hivo vitu muhimusana. Yafuatayo ni moja ya hayo mambo yatakayokufanya application yako itupiliwe mbali, na hutakaa uje kuitwa kwenye interview kama hutoyazingatia.

(a). Kutuma Application kwa ku-forward email
(b). Kutoandika subject kwenye email yako
(c). Kusahau ku attach relevant documents kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi
(d). Ku resend Email Application mbapo unakuta ulisahauku. Kama ulisahau ku attach documents, ni bora kutuma email mpya

NOTE: Kutokana na janga la ukosefu wa ajira, waajiri huwa wanapokea applications nyingi sana kiasi kwamba sio rahisi wakapitia applications zote katika zoezi la shortlisting. Hivyo, njia pekee wanayoitumia ni kutufa applications zote ambazo hazijazingatia professional application format na kubakiza zile ambazo ziko in good format, ndipo sasa waanze kuchambua nani ana sifa tunazozitaka.

Hivyo, unaweza kukuta una sifa zinazotakiwa, lakini kwakuwa hukufuata a professional appliaction format, application yako inatupiliwa mbali na unakosa kazi ambayo huenda wewe ndio ulikuwa candidate sahihi unayetakiwa.

Ni hayo tu kwa Leo. By professional I Am not an HR, hivyo I stand to be corrected na kuruhusu professionals wengine kuongeza mchango wako katika haya machache niliyoyagusia.

Asanteni sana.
 
Upo Sahihi kabisa mkuu.

Na kingine ningependa kuongeza, Mtu unatakiwa Kusoma Job description ya Tangazo la kazi na wewe uweke kwenye CV yako kuwa ndio vitu ulikuwa unafanya kwenye previous job ,

Hii inasaidia mwajiri kuvutiwa na ww kuwa ndio mtu anayemtafuta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom