Akasankara
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 4,268
- 5,815
Sasa unapouliza hayo maswali nani ayajibu?Kuna mambo yanaleta ukakasi.
Mashehe wa Zanzibar walikamatwa wakati wa Rais Kikwete, Lowassa hakusema chochote, na kipindi hicho Tanzania haikuwa na tatizo la Kibiti. Watu zaidi ya 30 wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha, halafu anaibuka Lowassa ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu anawakusanya Waislam nyumbani kwake na kuwaambia "WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA". Lowassa anakwenda mbele zaidi na kuwakumbusha namna 'watu walivyotumia dini kuleta machafuko wakati wa Rais Mwinyi.
Maswali ya kujiuliza,
1. Mbali na maagizo aliyotoa hadharani, Lowassa amekuwa anafanya nini nyuma ya pazia?
2. Lowassa anajua nini kuhusu Kibiti?
3. Lowassa ana maana gani anapoagiza waislam waongee 'lugha ambayo serikali inaielewa? Hiyo lugha ikoje?
4. Ni kwanini ametolea mfano wa mchafuko ya kidini wakati wa Mzee Mwinyi?
5. 'Shehe' ambaye amekuwa anafuatana na Lowassa kila mahali (hata leo alikuwa naye) ni kwa ajili ya maombi au ndiye msimamizi mkuu wa 'lugha' ambayo Lowassa anataka waislam waitumie.
Kuna tatizo kubwa.
Ndugu kuelewa ni karama, si rahisi kama unavyo dhani. CCM imewagharimu takriban miaka 20 kuelewa Lissu"....msiwe baridi........."-E.L.
sikiliza kuanzia 1.44 na shirikisha kidogo akili utamuelewa!
Ndugu kuelewa ni karama, si rahisi kama unavyo dhani. CCM imewagharimu takriban miaka 20 kumwelewa Lissu"....msiwe baridi........."-E.L.
sikiliza kuanzia 1.44 na shirikisha kidogo akili utamuelewa!
Lowassa kasema kila mtu atafsiri vile anavyoweza kutafsiri. Kwa lugha nyepesi ametoa kauli tata. Kiongozi mkubwa kama yeye anapotoa kauli tata maanake mara zote huwa zinalenga uvunjifu wa AmaniYa kujilipua ni mawazo yako. Lugha inaweza kuwa ya kwenda UN, AU kutoa malalamiko. Mahakamani kudai wafikishwa mahakamani/ kesi ifutwe etc! Kwa nini mnakimbilia kwenye upuuzi wa kujilipua. Unadhani Lowasa anaweza kuwa na mawazo ya kujilipua?
Hakuna tatizo kubwa ila tunang'ang'aniza tuone kuwa tunatatizo.Hebu rudia tena, it's as if you're talking sense.
TANZABASHITE wewe mnapenda kufikiria uchafu kwa kuwa mmezoea kuonea....sasa mnaogopa maneno mkianza kupigwa risasi km kibiti mtasema mmeshindwa
Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunakemea na kulaani kurudi kwa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.
Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameombea zirudi siku zile za taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.
Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.
Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala Shehe wala Kadinari wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.
Lowassa kasema kila mtu atafsiri vile anavyoweza kutafsiri. Kwa lugha nyepesi ametoa kauli tata. Kiongozi mkubwa kama yeye anapotoa kauli tata maanake mara zote huwa zinalenga uvunjifu wa Amani
Kwa Haya yanaoendelea dhidi ya Masheikh,nitashangaa sana kama kuna muislam anayejielewa ataipa kura ccm!!!Gwajima karopoka haswa lakini hajaguswa.Wazanzibar wameshaikataa ccm siku nyingi