Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 610
Hili sio jambo zuri sio tu kimaadili bali hata kisheria;kuishi na mke/mme wa mtu kabla hajapata talaka halali toka kwenye mahakama za kisheria ni kosa ndani ya katiba yetu!
Lkn nimeshtuka zaidi inaposemwa kuwa ukikaa na mke/mme wa mtu basi usipewe kura kwenye chaguzi na hivyo HAUFAI kuwa Rais wa TZ;hapo ndipo tunapopingana na wengine;Matatizo ya ndoa yanazungumzika ndani na nje ya mahakama(kama ambavyo mme huyu anataka fidia ya bilion 1 ili amuachie Slaa mwana mama huyu) lkn kufanya watz wote waufaidi uchumi wao inabidi achaguliwe kiongozi mwenye nia ya dhati ya kufanya hivyo!
Je sasa tuanze kujikita kwenye kuzungumzia suala la ndoa ya Slaa tukiacha kujadili jinsi ambavyo TZ ya mika 5 ya JK ilivyopteza dira?Je huu sio mpango wa CCM wa kuona watz tunapoteza muda wa kutowabana kwa nini hamna maisha bora hadi sasa kama walivyotuhaidi?
Tusiishie hapo tu kwenye kuishi na mtu ambaye bado ndoa yake haijavunjwa kisheria. Je ni sawa (kama tunavyosikia kuhusu Kikwete) kwa mtu aliye kwenye ndoa kutoka nje ya ndoa yake na kutembea kimapenzi na watu wengine?
Manake sasa huko tunakoelekea ni kubaya. Tutakosa hata anayetufaa kwani asiye na dhambi hizi na awe wa kwanza kumnyooshea mwenzake kidole....
Kiranga sidhani kuna anayetetea infidelity hapa.
Namshukuru sana MMJ maana hainiingii akilini mwenzio amekuaga, amekukimbia kwa zaidi ya miezi sita na hujafuatilia hata mara moja, leo unaibuka na madai umenyanganywa mke.
Kwa desturi zetu za kiafrika, kama amekutoroka, unakwenda kwao kutoa taarifa, na aghalabu unarudishiwa mahari.
Pili, naona hao waliochonga ngoma hii wameharakisha mno kama walivyokwisha sema wengine hapa, Mh ametoa taarifa tu kuwa yeye ni Mchumba wake; hawajaoona bado.
Shida ya Slaa ni kusema mno! Na hata huyo Josephine! Ingetosha kubaki pale kwamba wao ni wachumba,
lakini kusema kwamba wameishi tena kinyumba sasa hii wapi na wapi, bwana. Si sahihi na siwezi nikaacha kulikemea hili. Lakini nisipoambiwa kama nilivyoambiwa nitabaki nasema lakini washenzi hawa wameshaonjana, lakini sitaenda mbali, maana kwa namna fulani ni kama jamii yetu ya sasa imeshakubali kama desturi kwamba huwezi ukawa na mchumba bila ya kumfanya hawara(concubine). Hii ni bahati mbaya sana.
Mimi nadhani twendelee na kile tulichotaka kufanya, uchaguzi, haya ni mambo yameletwa kututoa kwenye mstari na wamefanikiwa kweli!!!! na inauma
Duh mkuu wangu ina maana Bongo hakuna ku register ndoa serikalini, kile cheti cha msikitini/kanisani ndio imetoka! basi itakuwa kazi sana kuthibitisha chochote maadam serikali hai register ndoa ina maana swala hili haliwezi kuwa la kisheria serikalini isipokuwa lihukumiwe kanisani..Mkandara usitake nicheke, Slaa kama rijali! Well nakubaliana sana na wewe, huu ni msimamo wangu pia. Ila labda masahihisho kidogo katika posting yako, ndoa za msikitini na kanisani zinatolewa hati ile ile ya serikalini, maana yake huna haja ya kwenda kuisajili serikalini, zinakubalika hivyo. Ila huyu chemba alikuwa na kimwana kinamburidisha mahali akajisahau ana familia, na familia ilivyo ondoka hakujua iko wapi, mpaka aliposikia Slaa anatangaza uchumba, na bado haikumwingia akilini hadi huyo mgombea diwani alivyokwenda kumwomba wampeleke kesi mahakamani ili wapate Bilioni moja!
Unajua kuna kitu nimejifunza sana kwenye siasa za Marekani. Unafiki haukatazwi kwenye siasa. Nakumbuka wakati Bill Clinton ana kashfa yake na Monica Lewinsky. Kuna watu wa GOP walikuwa mstari wa mbele sana katika kukemea utovu wake wa maadili achilia mbali kuapa kiapo cha uongo maana hili lilikuwa la kisheria zaidi.
Fast forward miaka kadhaa watu hao hao waliokuwa wakimkemea kumbe na wao ni watovu wa maadili kushinda hata yeye. Tena wengine walikuwa ni magay na wakabambwa waki-solicit uroda kwenye viwanja vya ndege.
Haya mambo bana ni magumu sana. Ngoja mimi nijinyamazie tu...
Mkuu hapa umeenda nje. Dr Slaa kamtangaza bibie woote mumemwona na tunajua kinachoendelea. Nafikiri mjamaa baada ya kuliona toto ktk luninga liking'aa akaingiwa tamaa mpya lakini jamaa alisha vuamahusiano kwa miezi sita hata asijali alipo mkewe.Nyani,
Nitakusoma sawa nikisema kwamba unasema kwamba unafiki haukatazwi katika siasa, na kwamba wale wale waliokuwa wanampigia kelele Kikwete na uongozi wa CCM kwa unafiki na ufisadi na wao wanakamatwa with pants down kwa habari za unafiki na ufisadi ?
Kwamba Slaa aliyepiga kelele sana kuhusu ufisadi wa EPA na yeye ni fisadi tu? Tena wa kuiba mke wa mtu ?
Nyani,
Nitakusoma sawa nikisema kwamba unasema kwamba unafiki haukatazwi katika siasa, na kwamba wale wale waliokuwa wanampigia kelele Kikwete na uongozi wa CCM kwa unafiki na ufisadi na wao wanakamatwa with pants down kwa habari za unafiki na ufisadi ?
Kwamba Slaa aliyepiga kelele sana kuhusu ufisadi wa EPA na yeye ni fisadi tu? Tena wa kuiba mke wa mtu ?
Mkuu toka lini tumefuata maisha ya viongozi wetu kuwa msingi wa mila na desturi za mwafrika au Mtanzania ktk siasa?.. Je, unataka watu wazungumze kuhusu maisha ya JK na wale waliomtangulia au yale ya Mkapa hayatoshi kuonyesha kwamba kiongozi anaweza kuishi na mke wa mtu aloachika.
Na kama kweli tunataka kuchukua haramu kulingana na dini basi kwa fikra zako unafikiria JK msafi, na hata tukianzia Nyerere utakuta mengi yanayo karibiana na hili yapo. Tena basi tukianza kudai kujua watoto wa hawa viongozi wetu nje ya ndoa jambo ambalo ni kubwa zaidi sidhani kaa atabakia mtu hata huko bungeni.
Maadam hili sii jambo kubwa ktk mazingira yetu hata kama ndio sababu ya kudumaa kwa uchumi wetu basi la kufanya ni kuweka sheria. Na zaidi ya hapo hata kama Dr.Slaa amefanya makosa bado ni kesi ya madai (civil case) ambayo kwa mila na desturi zetu talaka haina maandishi ila unampomfukuza mke ndio imetoka kama hujasajili ndoa hiyo.
Huyu jamaa anaweza kabisa kuwa hakusajili ndoa yake ktk vyombo vya serikali laa sivyo angeweza kuitoa na kuonyesha usajili wa ndoa yake ili hata hizo mahakama zifanye kazi yake kisheria. ndoa zinazotolewa hati na makanisa au misikiti sio uthibitisho wqa kupelekwa mahakamani kwani inaweza kuandikwa siku yoyote na ikarudishwa tarehe nyuma. Ni usajili tu wa kisheria unaoweza kumfunga Bibie ikiwa pia hakuna separation ambayo pia inampa ruksa bibie kutafuta maisha mapya. Kabla ya talaka Dr. Slaa haruhusiwi kumwoa huyo bibie lakini kupiga anaweza kabisa kupiga na halali wakiwa separate na mumewe.
Kimsingi huyu jamaa kesi kama hii inamweka yeye kkatika hali ngumu zaidi ikiwa mama huyu atathibitisha alivyokuwa abused na mtajwa ikabidi aingie mitini. Na kwa desturi za kibongo kama jamaa alikuwa na kipapi kingine wakati bibie akiondoka haikumwingia akilini kabisa kwamba ndio kavunja ndoa yake. Na Dr.Slaa kama mwokozi akachukua wajibu wa mwanamme rijali..
Huu ushabiki unatupeleka pabaya, let's be serious!!
Tatizo kubwa lililoifikisha nchi hii hapa ilipo ni kulindana na kuwaabudu viongozi ata pale ambapo makosa yao yapo dhahiri.
Nasikitika kuwa katika karne ya 21 bado watanzania wanaelekea kwenye njia hiyo ya ujima.
Dhana ya kuiba mke au mume naikataa. Haipo. Huyo mwanamke kaingia kwenye mahusiano na Slaa kwa hiyari na ridhaa yake mwenyewe. Kama kaibwa si arudi huko alikoibiwa? Kinachomzuia ni nini? Kwani kafungwa kamba?
Mume au mke huwa haibwi kwani mume au mke si mali (property). Kwa hiyo nakataa mlinganisho wako wa wizi za mali za umma na mambo
ya kimapenzi ambayo wengi wetu huridhia kuingia.
Labda nikujibu la mwisho kwanza.. Dr.Slaa hawezi kunichukulia mke wangu kwa sababu najua haya maji marefu hayawezi hilo moja..Labda niwe nimesha mtema mke wangu, tena basi bado naweza kuchukua vile vile akiwa naye yaani ningesubiri hadi Dr.Slaa anaingia Ikulu kisha nabembea na mali zangu kiulainiiiii..Haaa! haaa! haaa!Mazee Bob,
Mimi sikufuatilia maisha ya ndoa ya Slaa, najaribu kukaa as far na kitu chochote chenye maandishi au hata harufu ya ndoa, maana mimi na ndoa ni kama mafuta na maji, hatuchanganyiki.
Lakini washabiki wa Slaa wamekuja wenyewe na kulileta hili, wakimuimbia Slaa mashairi ya kubeza watu kama kitendo alichofanya ni cha kishujaa cha kupigiwa mfano kama ushindi wa vita wa Daudi wa waisraeli, au Achilles wa Wagiriki wa kale.
Hivi haya mambo ya aibu kabisa, ya mwanamme mmoja kumchukua mke wa mwanamme mwingine kinyumba, tunayaona ni ya kuyashangilia?
All because of politics?
Mwanakijiji this is an all time low. I am sorry.
Ina maana na wewe kama mwanamme Dr. Slaa akikuchukulia mkeo kwa style hii utasema "hajakuibia amekuzidi tu" na utamuimbia mashairi kumsifu ?
Labda si kuiba exactly as much as it is kuingilia/ violate mahusiano ya watu. Hili halibadilishi maudhui ya msingi ya criticism yangu.
Hapa natofautiana kidogo na wewe kuhusu maadili hasa yahusuyo mahusiano. Hii ni kwa sababu washiriki wote ni watu wazima na wanaridhia na kukubaliana watakayofanya na wanayofanya. Ingekuwa Slaa anatuhumiwa kulawiti watoto wadogo hapo ningechachamaa.Huwezi kuwa na tabia za kuvunja vunja maadili za kishenzi shenzi kama kuingilia ndoa za watu halafu ukataka watu wastaarabu wakupe kura zao uwe rais wao.
Hapana Kiranga, siyo madudu yale yale tu. Hawa wapinzani hawajaiba na kufuja mali za umma. Mimi niko radhi lijitu/ likiongozi liwe lizinifu tani yake lakini ikija kwenye mali, rasilimali, na maslahi ya wote lina miiko na maadili mazuri basi hayo mengine ya chumbani sijui limelala na nani sitajali sana. Nikienda pale Amana na kukuta hakuna mzazi aliyelala chini baada ya kujifungua, nikienda kule Mchikichini hakuna mtoto anayekalia gogo, jiwe, au tofali darasani basi sitajali sana hilo likiongozi sijui limemtokea demu gani.Sisemi kwamba huko upande mwingine wako any better, lakini hawa upinzani si ndio tumaini letu la mabadiliko na tulifikiri watakuja na chaguo bora zaidi? Mbona tunaona madudu yale yale tu ?
Labda nikujibu la mwisho kwanza.. Dr.Slaa hawezi kunichukulia mke wangu kwa sababu najua haya maji marefu hayawezi hilo moja..Labda niwe nimesha mtema mke wangu, tena basi bado naweza kuchukua vile vile akiwa naye yaani ningesubiri hadi Dr.Slaa anaingia Ikulu kisha nabembea na mali zangu kiulainiiiii..Haaa! haaa! haaa!
Pili turudi ktk siasa..Swala hapa ni kutazama hali halisi kwani sii Dr.Slaa aliyepelekea malalamiko au washabiki wake. Binafsi mimi nimetazama hali halisi na kugundua kwamba huyu jamaa alimwacha bibie aondoke kwake na asijue hata aliko kwa miezi sita (jambo ambalo linamfunga yeye kama mume. Kisha akajulishwa na mwanaye miaka 7 kuwa sasa wanaishi na BABA ikiwa na maana huyu jamaa hata child support alikuwa hatoi wala hajui maisha ya mwanaye na mkewe hadi hivi majuzi alipogundua kwamba huyo mkewe anaishi na Dr.Slaa. Hii kimila ina maana jamaa alim neglect mke na kibaya zaidi hata asiwafahamishe Polisi au usalama kuhusiana na hofu ya maisha ya mkewe. Angekuwa kauawa mjinga huyu asingekubali kwamba bado wapo kwenye ndoa ila hajui chochote kwani waliachana zamani kama miezi sita ilopita.
Upande mwingine hatufahamu Dr.Slaa amekutana na huyu bibie toka lini ila kwa taarifa ndogo tuliyokuwa nayo inaonyesha mtoto huyu nditye kamjulisha baba yake kwamba Siku hizi tunaishi na Daddy! ikiwa na maana muda wote wa nyuma haikuwa hivyo kama huyu jamaa alikuwa akiwasiliana na mwanaye.
Kwa hiyo, mimin sioni tatizo maadam huyu jamaa alimtema mwanamke hiyo homa ya kushtaki inatoka wapi.
Is Dr. Slaa ready for the prime time? Hatutaki kumpa urais halafu tukawa laughingstock of the world kwa sababu rais wetu mtu wa ajabu.
Hapo wala sina ubishi na nina maoni kama yako. Si vizuri kabisa kujihusisha na mtu ambaye bado yuko kwenye ndoa hata kama ndoa yake imetetereka. Sitaita 'kuingilia' bali naona ni kama kujihusisha (involve) zaidi na mtu aliye bado kwenye ndoa.
Hapa natofautiana kidogo na wewe kuhusu maadili hasa yahusuyo mahusiano. Hii ni kwa sababu washiriki wote ni watu wazima na wanaridhia na kukubaliana watakayofanya na wanayofanya. Ingekuwa Slaa anatuhumiwa kulawiti watoto wadogo hapo ningechachamaa.
Hapana Kiranga, siyo madudu yale yale tu. Hawa wapinzani hawajaiba na kufuja mali za umma. Mimi niko radhi lijitu/ likiongozi liwe lizinifu tani yake lakini ikija kwenye mali, rasilimali, na maslahi ya wote lina miiko na maadili mazuri basi hayo mengine ya chumbani sijui limelala na nani sitajali sana. Nikienda pale Amana na kukuta hakuna mzazi aliyelala chini baada ya kujifungua, nikienda kule Mchikichini hakuna mtoto anayekalia gogo, jiwe, au tofali darasani basi sitajali sana hilo likiongozi sijui limemtokea demu gani.