Video: Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akinaswa kibao na mwananchi

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
156
500
Watu wawili wametiwa mbaroni wakihusishwa na tukio la kumpiga kofi Rais wa Ufaransa, Emmanuel macron alipokuwa katika ziara rasmi Kusini mwa Taifa hilo.

Katika video inayosambaa mitandaoni, mtu huyo anaonekana kumchapa Rais Macron kabla ya kudhibitiwa na maafisa usalama, wakifanikiwa kumwondoa Rais, huku maneno “U-Macron uondoke” yakisikika.


Rais Macron yupo ziarani akitembelea maeneo mbalimbali ya Ufaransa, ziara yake ikitajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa kuwa ni siku moja tu kabla ya taifa hilo kuruhusu kufunguliwa kwa migahawa na baa baada ya kufungwa kwa miezi 7 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Rais Macron ataendelea na ziara yake katika eneo hilo siku ya kesho.

Chanzo: BBC
 

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
22,439
2,000
Nakumbuka Mwinyi akiwa kishastaafu alichezea kibao pale Diamond Jubilee... na akamsamehe yule jamaa

Laiti ingekuwa mwendakuzimu... hakyamama pangechimbika! Jamaa angepotea kama Azory Gwanda au Ben Saanane

Ila Yule jamaa alikula kisago heavy baada ya pale hadi kupelekea ukichaa na baadae mauti ingawa mhusika Mwinyi alimsamehe
 

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
762
2,000
Nakumbuka Mwinyi akiwa kishastaafu alichezea kibao pale Diamond Jubilee... na akamsamehe yule jamaa

Laiti ingekuwa mwendakuzimu... hakyamama pangechimbika! Jamaa angepotea kama Azory Gwanda au Ben Saanane
Na angepotea kweli.

Unawezaje kumpiga Kibao Amiri Jeshi kama hautafuti kifo?

Mimi mwenyewe tu nisingekubali. Ningekushughulikia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom