VIDEO: Nape akiongelea hatua ya Lowassa kuhama Chama

VIDEO: Nape akiongelea hatua ya Lowassa kuhama Chama

Wananchi wote wanajua ...Nape kafunga goli la mkono mtama...ametoa rushwa...apite kwenye ubunge
 
The coward normally have fake confidence...! Muangalie vizuri na kumsikiliza kwa umakini kwa sisi psychologists it's easy kujua ni muoga kiasi gani.
 
CCM Oyeeeeee. Hiyo ndio CCM ninayoijua subirini 25 oct 2015.
 
Huu utani. Nape hajui anenalo na anastahili msamaha
 
Tutaona mwaka huu ndo mwisho wa CCM vinginevyo......
 
familia ya mfale juha(ccm)wako kama familia ya kambare baba sharubu,mama sharubu,watoto sharubu..baba lao lenyewe zee la kucheka nakuwaza safari zenye per diem ndefu ndefu
 
Wako wanaotaka uongozi na wako wanaotaka kuongoza watu.Sasa hapa bwana Lowassa anataka uongozi na ndio maana alipokosa fursa CCM akamnunua Mbowe na kuhamia CHADEMA.

.
Mbona kama gakuna tofauti kati ya kutaka uongozi na kutaka kuongoza?
Huko mtama alikobambwa na rushwa alikua anatani nini, uongozi au kuongoza?.
.
 
Huu ni ubuyu wa kawaida tu sijui ni wa zanzibar au lah!! Acha waendelee kutambiana siku zisonge ila hapo hamna msafi wala jipya. mdomo ni mali yake.
 
Aliyekulia katika misingi ya dhuluma, udanganyifu na ulaghai atahubiri hayo hayo. Huyu ni mmoja wao, anaweza kuwaita waandishi na kuwaambia tutaiba kura bila hata woga wowote. Anawasema wanaotaka uongozi asema pia na wanaoshikwa mikono watumikie kikundi cha watu Fulani kwa kuwachafua wengine. Sijawahi msikia huyu akileta hoja za msingi zaidi ya kuonesha dharau akijivunia mamlaka aliyopewa. Mimi si mzungumzaji mzuri ila Nina hakika huyu hawezi kunishinda kujenga hoja.
 
Kama kawaida, majibu mepesi kwenye issue ngumu. Angeulizwa kwanini chama/serikali haitaki kujibu tuhuma za mamlaka ya juu kuhusika na Richmond? Haoni hii inakichafua chama na Mamlaka ya juu ya serikali? Na haoni swala hili kama ni la uongo, basi litakuwa linamsafisha Edward Lowasa na Kuichafua serikali na mamlaka yake ya juu?

Swali la kizushi: Kama katibu kiongozi anamjibu Waziri mkuu kuwa mamlaka ya juu imeridhia mkataba dhulumishi wa Richmond. Kiuhalisia kwa upembuzi mdogo tunajiridhisha hayo mamlaka ya juu yaliyo juu ya katibu mkuu na Waziri mkuu, yatakuwa ni Rais na Makamu wake. Sasa wananchi tumebaki na kubwa la kujiuliza huku tukiendelea kukosa imani na serikali hii.
 
Tunangoja kipenga cha tume kuwa Kampeni imeanza halafu tutakutana dimbani. Hapo ukweli wote utajulikana. Sipati picha!
 
Back
Top Bottom