Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Roma akiongea baada ya kutoka hospitali ya Mwananyamala. Amesema yeye na wenzake ni wazima wa afya, kimwili na kiakili na kuwashukuru watanzania wote waliowapigania kipindi cha sintofahamu yao.
Roma amesema kutokana na masuala ya makubaliano yao ya kuachiwa, wameomba kupumzika leo na kesho kisha Jumatatu wataongea kwa kina yote yaliyowapata.