VIDEO: Mkalimani aliyeingiza watu "Chemba"

VIDEO: Mkalimani aliyeingiza watu "Chemba"

Kiingereza mna kithamini, kiswahili lugha mama mnakidharau. Hii imekaaje!

Mswahili akijua kuongea kiingereza humwambii kitu, ni kama kapewa dunia yote amiliki 😂
Hata hao wasiojua Kiswahili pia nao wakikijua hata kidogo tu basi huhisi raha wakizungumza na wenyeji. Sasa vivyo hivyo ndivyo sisi tusiojua kiingereza, tunajihisi. Hakuna anayedharau lugha ya mama. Huko nje ya nchi mkikutana waswahili mbona raha kwani ndio huboeki tena kama ingekuwa twakitukuza sana hicho kiingereza chao basi hata tukiwa ughaibuni tungekuwa bado tunalonga hiyo lugha sisi kwa sisi waswahili. Au nimedanganya hapo?
✌️
 
Jibu hilo hapo.
8791d6925df043ef9c6459ad84dfc3ce.jpg
 
Kuambiwa jiwe hakuwa mpenda safari ni tusi hilo, duh?
Halafu ujue hakuna vile utasema walinda image ya taifa au rais wakati wewe ni mkalimani, hivi huo umati wote hapo kwani alifikiri yeye ndiye anayejua kiswahili ndio akafanya 'blunder' hiyo. Sema tu alikosea ka binadamu wengine, na ilimpasa asikilize kwa umakini, yule anayeongea ni Rais kama mwingine na asingeweza kutoa neno bovu kwa nchi, raia au hata hayati wakati yeye mwenyewe kaalikwa. Nafkiri umenipata, yule jamaa kateleza tu
✌️
 
Mkuu, asante kwa taarifa.

Maoni yangu, kama kiingereza unakijua, na umeelewe kilichosemwa, tafsiri ya kiswahili inakuhusu nini? "Shauri yao wasiojua kiingereza".

Pia, kama tafsiri ya maneno haipo sawa kabisa na maneno yaliyotamkwa, lakini tafsiri hiyo haiathiri mawasiliano yanayoendelea, kuna tatizo gani? "Shauri yao wasiojua lugha hiyo"

Halafu, kwa nini kuzogoa makosa ya tafsiri ya 'english - swahili', ile ya french - swahili' mliielewa vizuri?

Wanadiplomasia wamesema, kuna ukakasi kwa maneno yaliyosemwa, hivyo haikuwa busara kwa mkalimani kuyatafsiri kama yalivyotolewa. Mfano, ukitukanwa kichina, wakati kichina hukijui, mkalimani wako akatafsiri kuwa unasifiwa, wewe ni mtu mzuri, si ndio busara na diplomasia yenyewe?

Hapo ndio utawatambua wabongo na kuwavulia kofia kwa ujuwaji. Wale waliosema damu itamwagika TZ watasubiri sana.
 
Sasa kama huyo mchina akisema kwa kichina kuwa "kamfinyeni huyu huko mbele!" Halafu mkaliman atafsiri kinyume huoni kuwa maana ya ukalimani inapotea?
Diplomasia alipaswa kunyamaza na kusubiri maneno yaliyo fuata!

Kuongopa siyo diplomasia
 
Tambua ule ni mfano tu. Hapa ni suala lingine ambalo pia ni mfano tu . Sasa unataka tuanze kubishana kutokana na mifano!
 
Mwenyekiti wa kamati ya maziko alikosea kumpa shavu yule bwana mkalimani ni aibu kubwa kwa taifa letu na ninaomba anaemfahamu mkalimani amuanike hapa
 
Mkaliman kaks sana LEO KAHOJIWA CLOUDS Leo tena kasema alitumia Clues kutafsili
 
Back
Top Bottom