VIDEO - MIUJIZA nchini Haiti, Aokolewa Siku ya 27 Baada ya Kuzikwa na Kifusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - MIUJIZA nchini Haiti, Aokolewa Siku ya 27 Baada ya Kuzikwa na Kifusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,911
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Evans alipookolewa baada ya kuishi siku 27 akiwa amefunikwa na kifusi cha nyumba aliyokuwemo Wednesday, February 10, 2010 1:38 AM
  Miujiza imetokea nchini Haiti kwa mwanaume ambaye alikuwa hana chakula wala maji kuweza kuokolewa toka kwenye kifusi cha jumba alilokuwemo siku 27 baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo wakati tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea nchini Haiti. Madaktari nchini Haiti wanampatia matibabu mwanaume mwenye umri wa miaka 28 wa nchini Haiti ambaye ameokolewa toka kwenye kifusi cha jengo alilokuwemo siku 27 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti januari 12 mwaka huu.

  Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Evans Monsigrace, aliokolewa jana jumanne na aliwaambia madaktari kuwa alifunikwa na kifusi cha nyumba aliyokuwemo wakati alipokuwa akipika wali.

  "Kimaajabu ameweza kuishi 27 chini ya kifusi cha nyumba yake", alisema daktari Dushyantha Jayaweera, mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa mwanaume huyo.

  Kwa mujibu wa mama yake Evans, Evans aliokolewa baada ya kugunduliwa na watu waliokuwa wakiondoa kifusi cha nyumba hiyo.

  Dokta Jayaweera alisema kuwa Evans alioneka kuwa dhoofu sana na kama amechanganyikiwa vile lakini ogani zake zote zilionekana kuwa salama.

  Evans aliwaambia madaktari kuwa aliishi chini ya kifusi kwa muda wote huo bila maji wala chakula na kuwafanya madaktari watume wataalamu kwenye eneo alilookolewa kuthibitisha madai yake.

  Wataalamu hao walishindwa kugundua uwepo wa maji au chakula kwenye eneo hilo na kuwafanya madaktari waumize vichwa wasijue imekuwaje Evans ameweza kuishi siku zote hizo bila kula wala kunywa maji.

  "Tukio lake limetufanya tuanze kufikiria upya yale tuliyokuwa tukiyajua kuhusiana na mwili wa binadamu", alisema dokta Jayaweera.

  Chini ni VIDEO ya tukio la kuokolewa kwa Evans.


  VIDEO - Miujiza Nchini Haiti  Bonyeza hapa kuiona Video http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4052658&&Cat=2
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ya Mungu mengi. siku zote tunajua kwa sehemu tu na kamwe hatujapata kujua jamb lolote kikamilifu. hao madaktari sasa watamrudia Mungu (kama walikuwa wanjidanganya na elimu zao kuwa hakuna Mungu)

  ni uthibitisho mwingine kuwa maisha ni zawadi itolewayo na Mungu pekee, hata waoendao hospitali na kupona, wanaponywa na Mungu!!!!!!!!

  Bwana ametenda makuu, jina la Bwana lihimidiwe..................
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Huyo survivor anasema alikuwa anapewa maji na mtu alievaa mavazi meupe ndo akasavaiv. Nadhani madaktari wakithibitisha mazingira alokuepo kwamba hakukuwa na uezekano wa kupatikana kwa maji na wala chakula, hii itakuwa fursa adimu kwa KIRANGA atupe somo na amalizie na SALA YA TOBA. :D
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Bila shaka amevaa kanzu ya kiislamu
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  mmh! not now, not now please!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,620
  Likes Received: 23,750
  Trophy Points: 280
  Pia Haiti ndio nchi inayoongoza kwa technolojia inayoitwa Voodooism, mi technolojia ya kiasili inayotumika kukufua wafu na kuwafanya waendelee kuishi kitabu cha "Make the Copse Walk" kinaeleza zaidi. Kwa vile misingi ya practice yake ni siri kubwa, mzungu kashindwa kuing'amua hivyo wanaitangaza voodooism kama uchawi uliopindukia.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...