VIDEO: Mahojiano na Mh. Zitto Kabwe katika Makutano Show

Makutano Show

Member
Aug 3, 2012
21
65
Wadau wa JF

Nawashukuru sana wote mliochangia katika kipindi cha kwanza cha Makutano kilichorushwa Magic FM kuanzia saa tisa mchana hadi kumi na mbili jioni kwa kumuuliza maswali Mheshimiwa Zitto Kabwe na pia kutoa maoni. Nilijaribu kadri ya uwezo wangu kumuuliza maswali yenu na aliyajibu.

Ushirikiano wenu na maoni yenu naamini yatakifanya kipindi kiwe bora zaidi hivyo usisite kunishauri au kunipa maoni ambayo unaamini yatakifanya kipindi cha Makutao kiendelee kuwa bora kadri siku zinavyozidi kwenda. Kila wiki tutakuwa na Mgeni na nitaendelea kupokea maswli yenu.

Kwa wale ambao hamkuweza kusikiliza kipindi siku hiyo clip za mahojiano zipo katika Youtube Channel ya kipindi unaweza kubofya hapa chini kusikiliza.

Fina



 

Attachments

  • 2.JPG
    2.JPG
    67.3 KB · Views: 548
  • 3.JPG
    3.JPG
    78.2 KB · Views: 568
Last edited by a moderator:
Ok tupo pamoja sana, next time ukiwa na kipindi tujulishe manake naona huku kwako kuna mwanga wa kweli wa mabadiliko, Ni lini tena unafanya kipindi? Halafu huwezi kupata airtime kwenye luninga/channel 10 ukawa live?
Wishn u all the best fina!!

Shukrani Sizinga

Kipindi ni kila Jumamosi kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili jioni. Kuhusu live kwenye TV ondoa shaka liko ndani ya mipango itakapokuwa tayari nitakufahamisha.

Asante sana.
 
wewe ni wa ukweli Fina na tunakuhakikishia kuwa kipindi chako kitakuwa na mvuto na kitaleta mageuzi makubwa ktk tasnia ya habari.keep it up achana na mawatu kama akina kibonde na semunyu manafiki makubwa.
 
hicho kipindi naweza sikiliza nikiwa online? naomba link.

hongera sana kwa kuanzisha kipindi hicho.....
 
wewe ni wa ukweli Fina na tunakuhakikishia kuwa kipindi chako kitakuwa na mvuto na kitaleta mageuzi makubwa ktk tasnia ya habari.keep it up achana na mawatu kama akina kibonde na semunyu manafiki makubwa.
------na Gerard Hando na Paul James! Kazi kusoma gazeti la Uhuru (binya pua) 'kongwe la Chama Cha Magamba'!
 
hicho kipindi naweza sikiliza nikiwa online? naomba link.

hongera sana kwa kuanzisha kipindi hicho.....

Edson

Website ya Magic FM inafanyiwa matengenzo kwa sasa lakini kabla ya kipindi kingine Jumamosi itakuwa hewani na tutaiweka hapa ili wadau wote muweze kusikiliza.

 
Huyu dada namkubali sana hata alipokuwa kwenye ile radio ana vitu fulani hata akiwa anaongea unamsikia akiwa anaamaanisha siyowasigizaji ambao wamejaa mizaa hata kwenye mambo ya msingi. kama utaendelea hivi utapata support kubwa kwenye jamii maana jamii hivi sasa inataka mtu mkweli siyo waigizaji
 
Fina,

Vipi unaweza pia ukamjumuisha Kipanya katika kipindi? Manake nyie wawili mkiwa pamoja mnafanya kazi nzuri sana...rejea enzi zile mkiwa pamoja pale radioni.

Hongera sana na pia uzidi kukaza mwendo.
 
unatakiwa ufanye kama startv wanavyo fanya. anzisha maada hapa jf na useme mgeni nani halafu uwe unasoma moja kwa moja coment kutoka jf na utaje aliye uliza. mia
 
Back
Top Bottom