VIDEO - Maajabu ya Dunia - 'Mtu Nusu' Apata Mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Maajabu ya Dunia - 'Mtu Nusu' Apata Mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, Apr 29, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Kenny EasterdaySunday, April 04, 2010 4:18 AM
  Mwanaume wa nchini Marekani maarufu kama 'Half Man' ambaye maisha yake yote amekuwa akiishi akiwa na nusu ya mwili wake tu kuanzia kiunoni ametamba kuwa yeye ndiyo baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mchumba wake ingawa baadhi ya watu hawaamini kama kweli mtoto ni wake wakidai atakuwa kabambikiwa mtoto.Kenny Easterday mwanaume wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 35 ambaye ana nusu mwili kuanzia kiunoni, anasubiria majibu ya DNA ili kuwathibitishia watu kuwa yeye ndio baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mpenzi wake Nicky.

  Katika documentary mpya itakayorushwa hewani leo kwenye televisheni ya Marekani, Kenny mkazi wa West Virginia anasema kuwa yeye ndiye baba wa mtoto Desiree aliyezaa na mpenzi wake Nicky,33 miaka saba iliyopita.

  "Watu wanataka kujua kama Kenny ana sehemu za siri", alisema Nicky katika documentary hiyo itakayorushwa hewani na televisheni ya The Learning Channel (TLC).

  "Tunafanya mapenzi kama watu wengine, Kenny ana sehemu za siri kama mwanaume mwingine", aliongeza Nicky.

  Kenny alizaliwa akiwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana duniani unaoitwa sacral agenesis ambao huzuia uti wa mgongo kukua kama kawaida.

  Madaktari walilazimika kuikata miguu yake miwili iliyojipinda iliyojichomoza kidogo chini ya kiuno chake na kisha kuuchukua mfupa wa ugoko wake na kuutumia kuurefusha uti wa mgongo wake.

  Kenny ambaye kutembea kwake ni kwa kutumia mikono anasema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kupata mtoto.

  "Nataka niwe na mtoto atakayelibeba jina langu ambaye ataweza kusimama mbele ya watu na kusema 'HUYU NDIYO BABA YANGU'", alisema Kenny.

  Angalia VIDEO hii ya kustaajabisha inayoonyesha maisha ya kila siku ya Kenny.
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kweli hii kali.duh Duniani kuna maajabu.Nusu mtu duh .Mungu ni waajabu kweli.
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mbona siioni video!
   
 4. Ramwai

  Ramwai Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ni muweza yote,
  Acheni mamboya kumchunguza chunguza Kenny, huyo baby ni wake nadhani angekuwa hana jinsia hata mpenzi asingekuwa nae, mbona anaonekana yupo fit kabisa na ameumbika kiume haswaaaaaaaaaaa,
  Yaani tooso handsome
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Du kweli sifa na utukufu na wake yeye aketie katika kiti cha enzi
   
 7. M

  Makanyagio Senior Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii kali mwangu. Duh!
   
Loading...