Video: Kenyans scramble to buy cheap unga in a supermarket.

Mie najichekea tu
Sina wazo la unga mwaka mzima
Hahaha
Njaa mbaya
e0c931500effaaeecdfbb0a4f890bf7e.jpg
 
dah! this is one of the failures of the jubilee administration...food security...hivi watanzania si mtusaidie na mahindi jameni...jamaa hapa haswa wale wa magharibi ya kenya wanahangaika kwel kwel...:D:D:D
...Tutawasaidia, mahindi tayari yanakauka na mengi kweli msimu huu, poleni majirani.
 
Ugali wa Mahindi siyo asili ya Afrika, alileta Mzungu ktk the Americas, asili ya Afrika ni Mtama, Mihogo, n.k. kwanza Mahindi ni chakula cha Mifugo kwa Wazungu!

Mahindi asili yake Mexico, Mihogo ilianzia Brazil, Mtama asili yake Uchina hivyo hata wewe hapo ulichovaa mwilini asili yake Ulaya. Unavyokula na kunya vyote sio asili ya Kiafrika.
Hata hivyo nilichokisema ni kwamba Afrika tunapenda ugali.

Halafu sijui nani kawadanganya kwamba Kenya tunakula sembe kila maeneo, kuna wale tunakula dona kila siku, kwanza dona ndio hupikwa kwangu siku zote.
 
Kuna hitilafu kwenye distribution and value chain ya vyakula nchini mwetu. Hasa upande wa supply. Kwangu mie, huu ni mfano mzuri sana ya mbinu za wafanyi biashara wakiungana na baadhi ya taasisi za serikali kufanyisha uhaba wa bidhaa flani ili mradi wao wavune mamilioni. Wangelitabiri huu uhaba na kuingiza hayo mahindi ya Mexico miezi mbili tatu mapema. Masilahi ya wanjiku hapa hayana umuhimu. Wameweza kufanya hujuma kama hili na maziwa pia. Pesa linatakikana kwa haraka zaidi, na tusidaganyane hatujui kwa nini. Kwa wale walioishi Kenya hii, mnaweza pia kumbuka ule uhaba wa sukari miaka ya 90 na malengo yake yalikuwa yale yale.

Hata hivyo naomba tule pia mazao mengine. Tuige wenzetu wa afrika magharibi na tule pia yams(hili sijui wanaliitaje kwa kiswahili). Iconoclastes umetaja zao la yam kama limetokea nje ya afrika lakini sidhani. Limekuwa afrika magharibi enzi na maenzi.
 
True. Yams have been cultivated in Africa for thousands of years. I stand corrected.

Yam - New World Encyclopedia
 
Back
Top Bottom