Wakuu nahisi kwa hili tusaidiane mawazo
Mimi naomba kuuliza swali labda mnaweza kunitoa ushamba
Kwa nini TV za nje zinakuwa ni clear kuliko za Tanzania?
Mmeona hapo wakati anahojiwa JK picture quality ya STAR TV ilikuwa terrible itafkiri TVZ ya 1980's lakini once walipounganika na BBC London picha ikawa clear zaidi.
Najua mtakuja na hoja ohhh HD na kadhalika lakini ukitazama TV Channels za Kenya utaona quality ni kama za nchi zilizoendelea
Mbaya zaidi ni kuwa TV STATIONS ZOTE ZA TANZANIA PICTURE QUALITY ni mbaya sana...yaani unaona moshi moshi vivi
Swali langu la pili:
Kwa nini TV Stations za Tanzania hazina youtube channels? Hivi inamaana hakuna aliyejua kuwa kuna market ya kutisha ya matangazo online?
Natumai bwana Pasco na wengine mtanipa majibu
hawezi hata kujibu maswali? huyu mtu kweli janga la taifa
Sasa mkuu, itakuwa ni jambo la manufaa kama utaanzisha thread inayohusu swali lako maana hapa tunataka kumjadili kiongozi wetu na mahojiano mafupi aliyofanya na BBC swahili.
Samahani kama ntakuwa nimekukwaza maana hii ya mheshimiwa raisi wetu hapa naona hakujiandaa kwa maswali.
Interview ilikua nzuri tu kwa sababu raisi alijibu naswali aliyoulizwa kahiyo kama kuna tatizo basi ni kwa muulizaji. Kuna mambo mingine sio lazima yeye ayajue kama plastic kutengenezwa kutokana na gas sio lazima ajue kwani yeye sio mtaalam wa mambo hayo. Kumchukia mtu kutusifanye tukachukia kila kitu chake. Hakuna mtu ambae atakua anakosea sana kama yule atakaedhania kua rais anajua kila kitu, huo ndio uzembe mkubwa kuliko hiyo interview yote
Yaani huyu jamaa hata kemia ya mwanzo haipandi, eti plastiki ni gesi au alimaanisha kusema plastiki ni hydrocarbon,Sijaelewa chochote hapo,halafu plastic ni gesi?mhn!
Yaani huyu jamaa hata kemia ya mwanzo haipandi, eti plastiki ni gesi au alimaanisha kusema plastiki ni hydrocarbon,
Huyu kilaza sijui anaongelea nini? Analaumu nchi nyingine za kiafrika kuuza mafuta ghafi na kununua mafuta yaliyosafishwa. Mbona Tanzania inanunua hadi matunda tena artificial toka uarabuni wakati matunda yanaoza kila sehemu nchini? Kweli jamaa ni mbabaishaji na msanii mwenye kuota ndoto za mchana. Angalia alivyo hovyo anasema anashabikia New Castle ya Uingereza wakati ameua kila kitu hapa nchini. Kweli wanaohoji mantiki ya kumchagua hawajakosea. Jamaa ni mtupu mno hajui hata anachosema. Kweli Tanzania inaelekea kuzimu chini ya bongolala kama hii.