Nataka kufahamu uhalisia wa hii video ambayo inasemekana hii ni athari inayotokana na vita ya Israel na Iran na hapa inaonesha ni Israel baada ya kushambuliw na Iran ni kwel uhalisia hii video au potoshi?
Asante
Asante
- Tunachokijua
- Kuanzia Februari 28, 2026 vita kati ya Israel, Iran na Marekani iliibuka na hivyo kupelekea mzozo baina ya mataifa hayo, ambapo vite hiyo pia ilipelekea kifo cha Ayatollah Khamenei aliyekuwa kiongozi wa Iran.
Madai
Kumekuwa na video ikionesha majengo yakiwa yameshambuliwa na kuelezwa ni majengo ya Iran baada ya kushambuliwa na Israel.
Uhalisia wa video hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa video hiyo ni ya matukio yaliyotokea Gaza mwaka 2025.
Vyanzo mbalimbali ikiwemo the guardian walichapisha video za kufanana na hiyo inayoonesha kuwa maafa yaliyotokea Gaza wakati watu walipokuwa wakirudi makwao.
Itakumbukwa kuwa Israel ilifanya mashambulizi Gaza kulipiza kisasi na hivyo kuua zaidi ya watu 61,000 baada ya Hamas kuivamia Israel Oktoba 7, 2023 na kuu takribani watu 1,200 na kuwachukua wengine 251 kama mateka.