SI KWELI Video inaonesha bara la Afrika likigawanyika

SI KWELI Video inaonesha bara la Afrika likigawanyika

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hiki kipande cha video kilichoambatanishwa na ujumbe kuwa

"Hi Ndiyo Ile Tulisema Bala La Africa litajigawa, naona dalili zimeanza, tuliosoma Civics hii kitu tunaijua kitambo"

1761464261388.png

 
Tunachokijua
Kuna kipande cha video kinachosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kikionesha ardhi inagawanyika huku ikielezwa kuwa dalili za bara la Afrika kujigawa zimeshaanza kuonekana.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Kumekuwa na taarifa kutoka kwa wanasayansi na tafiti mbalimbali zikieleza kuwa bara la Afrika litakuwa kugawanyika vipande viwiili, gazeti la The Citizen mwaka 2023 liliripoti, ambapo mataifa ambayo kwa sasa hayana bahari yanaweza kuwa na fukwe za bahari mathalini Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Burundi, Malawi, na Zambia.
screenshot-2025-10-26-111213-png.3493785


Tovuti ya Economic times inaandika kuwa Ushahidi wa kijiolojia umeendelea kukusanywa kwa muda. Mtikisiko wa ardhi nchini Ethiopia ulisababisha ufa mkubwa mwaka 2005
screenshot-2025-10-26-105801-png.3493780

ukafuatwa na ufa mwingine nchini Kenya mwaka 2018.

screenshot-2025-10-26-110241-png.3493783
Wanasayansi sasa wanakadiria kwamba mgawanyiko kamili wa bara unaweza kutokea ndani ya kipindi cha kati ya miaka milioni moja hadi milioni tano, mapema kuliko ilivyodhaniwa awali.

Utafiti ujilikanao kwa jina la Investigation of the Africa splitting into two as new ocean forms. Geodesy and Cartography wa mwaka 2025 unaonesha kuwa Ingawa hilo litachukua kati ya miaka milioni tano hadi milioni kumi, bara hilo hatimaye litagawanyika kuwa mabara madogo mawili, na hivyo kuunda bonde jipya la bahari kati yake.

Aidha, ufuatiliaji wa zaidi umejirirdhisha kuwa video hiyo si halisi na badala yake imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde, licha ya kuwa na mapungufu mengine ikiwemo taarifa kutkutaja tukio limetokeawapi na lini.
screenshot-2025-10-26-102804-png.3493786
Back
Top Bottom