PreGE2025 VIDEO: Freeman Mbowe akitangaza agenda ya No reform No Elections, G55 Wanadhihirisha ule ulikuwa ni mchezo wa maigizo wa Mbowe

PreGE2025 VIDEO: Freeman Mbowe akitangaza agenda ya No reform No Elections, G55 Wanadhihirisha ule ulikuwa ni mchezo wa maigizo wa Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbiwe yeye aliongea lakini hakushinikiza mtu hicho alichoongea tofauti na Lisu yeye anashinikiza watu kuwa lazima no reform no election sio hiari na watu hawataki wanataka kugombea yeye kakomalia tu kuwa watake wasitake no reform no election ndio maana sasa hivi anaitwa dikteta uchwara
Wewe kilaza lile lilikuwa azimio la Mkutano Mkuu haliwezi kutenguiwa kwa hoja za mitandaoni.
 
Hakuna mtu namwonea huruma kama Catherine Ruge kwenye huo Mkumbo aisee,

Sasa atashuhudia Covid 19 wakirejea na yeye akitoweka inauma sana 😭😭
Unamwonea huruma mtu anayelamba milion 300 kwa mwezi 😁😁😁
Wewe.na yeye nani wa kuonewa huruma
 
Ukweli ni NO REFORM NO ELECTION.
Kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Tanzania.
Wewe si unachumia tumbo.
Wewe jamaq unaweza kuwa mmoja kati ya milioni moja ya wanaCCM ambao wanaijua kweli na wanaiweka wazi, tatizo tuu ni kweli haijakuweka huru!
Kongole kwa kumwambia ukweli huyo.

No Reforms,No Election ni kwa mustakabali mwema wa Tanzania, kwa wanaoipenda Tanzania kweli toka Moyoni.
 
Hii agenda ya no reforms no election ndio imebeba taswira nzima ya mapinduzi na mwelekeo mpya wa siasa ya nchi hii, ni agenda Moja nzito sanaa ambayo wakiweza kweli kuisimamia na ikafanikiwa hata kwa asilimia 60 basi tunakwenda kushuhudia mwelekeo mwingine kbs wa siasa zetu na taifa kwa ujumla.

Lissu na Chadema wategemee upinzani na uasi mkubwa sana kwenye hii agenda kwani watawala wanaojua kabisa hapo ndo turufu ya unyongaji wanaowafanyia( tume ya uchaguzi ya Rais) hivyo kuwalazimisha kufanya mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi maana yake unakuwa umetenganisha kichwa na kiwiliwili sasa hiyo haiwezi kuwa kazi ndogo
 
Lisu ndie kalibeba nchi nzima
Mbowe hajawahi zurura nalo nchi nzima aliongea tu kwenye hotuba yake na hajawahi peleka kikao chochote liwe approved
Lisu ndie kalivalia njuga wakati watia nia hawalitaki
kama watia nia hawataki waachwe waingie kwenye uchaguzi wakaangukie pua mbele ya ccm. Shida iko wapi? Wanaambiwa bila reform ni ngumu kushinda hawaelewi, waachwe waingie wakishindwa wasilalamike kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki
 
kama watia nia hawataki waachwe waingie kwenye uchaguzi wakaangukie pua mbele ya ccm. Shida iko wapi? Wanaambiwa bila reform ni ngumu kushinda hawaelewi, waachwe waingie wakishindwa wasilalamike kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki
Sahihi Sioni shida yeyote. Wak8shinda ni wao na wakishindwa ni wao

After all hawajaomba chama kiwasaidie kushinda au kushindwa
 
Back
Top Bottom