PreGE2025 VIDEO: Freeman Mbowe akitangaza agenda ya No reform No Elections, G55 Wanadhihirisha ule ulikuwa ni mchezo wa maigizo wa Mbowe

PreGE2025 VIDEO: Freeman Mbowe akitangaza agenda ya No reform No Elections, G55 Wanadhihirisha ule ulikuwa ni mchezo wa maigizo wa Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

PiedPiper77

Senior Member
Joined
Jan 8, 2025
Posts
180
Reaction score
223

Kuna wakati Watanzania tunaanza kuamini Freeman Mbowe alizungukwa na vijana hatari sana huku yeye akila na kulala nao.

Kama wanavyojitambulisha hawa vijana wanaojiita G55 ni vijana toka team iliyojitanabaisha kuwa ni team Mbowe wakati wa Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu.

Kama vijana hawa au boss wao Mbowe walikuwa ni waasisi wa No Reforms No Election na leo ni hao hao wanatoka tena hadharani na kupinga "No reforms No Election" kwa kisingizio walikuwa wanatishia nyau tuu,

Nadhani hiki ni kiwango Cha Juu kabisa Cha Ujinga walichonacho hawa wanasiasa.

Hata hivyo, Hawa vijana wa G55 wanaharibu kabisa image ya Freeman Mbowe na kuwafanya Watanzania waamini kuwa Mbowe alikuwa anafanya michezo ya kuigiza mingi ili kujipatia chochote toka kwa Watawala kama hiki wanachokisema vijana wake ni Cha Kweli,
 
Lisu ndie kalibeba nchi nzima
Mbowe hajawahi zurura nalo nchi nzima aliongea tu kwenye hotuba yake na hajawahi peleka kikao chochote liwe approved
Lisu ndie kalivalia njuga wakati watia nia hawalitaki
wacha tuone litaisha vp!!👿
 
Kwahiyo ni Kweli Mbowe alikuwa anaigiza?
Mbiwe yeye aliongea lakini hakushinikiza mtu hicho alichoongea tofauti na Lisu yeye anashinikiza watu kuwa lazima no reform no election sio hiari na watu hawataki wanataka kugombea yeye kakomalia tu kuwa watake wasitake no reform no election ndio maana sasa hivi anaitwa dikteta uchwara
 
View attachment 3293544
Kuna wakati unafika tunaanza kuamini kuwa Freeman Mbowe alizungukwa na vijana hatari sana huku yeye akila na kulala nao.

Hawa vijana wanaojiita G55 ni vijana toka team iliyojitanabaisha kuwa wao ni team Mbowe wakati wa Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu.

Kama vijana hawa walikuwa ni waasisi wa No Reforms No Election na Leo ni hao hao wanatoka hadharani na kuipinga eti kwa kisingizio walikuwa wanatishia nyau tuu nadhani hiki ni kiwango Cha Juu kabisa Cha Ujinga,

Hawa vijana wa G55 wanaharibu kabisa image ya Freeman Mbowe na kuwafanya Watanzania waamini kuwa Mbowe alikuwa anafanya michezo ya kuigiza mingi ili kujipatia chochote toka kwa Watawala.
lakin gentleman,
hata wewe fikiria vizuri.
hivi kweli wewe unaweza kunizuia mimi nisipige kura kwa hivyo ilivyo? surely?🐒
 
Lisu ndie kalibeba nchi nzima
Mbowe hajawahi zurura nalo nchi nzima aliongea tu kwenye hotuba yake na hajawahi peleka kikao chochote liwe approved
Lisu ndie kalivalia njuga wakati watia nia hawalitaki
Ukweli ni NO REFORM NO ELECTION.
Kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Tanzania.
Wewe si unachumia tumbo.
 
lakin gentleman,
hata wewe fikiria vizuri.
hivi kweli wewe unaweza kunizuia mimi nisipige kura kwa hivyo ilivyo? surely?🐒
Unafahamu kwanini mtu anapiga kura?
Moja ya sababu kubwa ni kumpenda Mgombea Sasa kama Mgombea hayupo kura za Nini?
 
Hao watia nia wanasahau dhuruma wanazofanyiwa wakati wa Uchaguzi!
Nadhani katika kupinga hiyo agenda ya No reform no election wangeeleza namna gani ambavyo Chadema ikishiriki watapambanaje na hizo dhuruma zinafanywa wakati wa uchaguzi zaidi ya kuususia!
 
Unafahamu kwanini mtu anapiga kura?
Moja ya sababu kubwa ni kumpenda Mgombea Sasa kama Mgombea hayupo kura za Nini?
katiba ya Tanzania inasema hivi,
The winner of an elections takes all.

Ni kwamba,
kwenye uchaguzi mkuu,
hata wakijitokeza wapiga kura wa3 tu nchi nzima, halafu akapatikana mgombea aliepata kura2,

atatangazwa mshindi kwa mujibu wa Sheria,
atakamata dola, ataunda Serikali na kuongoza nchi bila kelele wala mdomo wa kibaka au tapeli wa kisiasa nchini.

Mapenzi yako baki nayo moyoni mwako, uchaguzi ni suala la kikatiba 🐒
 
Naona kinachofanyika kwa sasa ni kujaribu kukigawa Chama ili kukisambaratisha!
 
Mbiwe yeye aliongea lakini hakushinikiza mtu hicho alichoongea tofauti na Lisu yeye anashinikiza watu kuwa lazima no reform no election sio hiari na watu hawataki wanataka kugombea yeye kakomalia tu kuwa watake wasitake no reform no election ndio maana sasa hivi anaitwa dikteta uchwara
Huna akili
 
Kwani huo msimamo hawawezi kuu review?? Kuona kama unafaa ama la..hyo siyo biblia
 
Mleta mada Achaneni na Mbowe alishaachia ngazi
Lisu na timu yake wajibu hao.G55

Waachane na Mbowe kumtaja taja
Hao G 55 mbona walishajibiwa kuwa azimio la No Reforms No Election lilipitishwa na kikao cha juu kabisa cha maamuzi yaani Mkutano Mkuu hivyo kama wanataka waitishe tena Mkutano Mkuu kutengua azimio hilo badala kuhangaika mitandaoni kama machizi.
 
Back
Top Bottom