Pazi na Jogoo
JF-Expert Member
- Aug 12, 2016
- 331
- 494
Wale wamekuja leo, kwa sauti za mbali zinasikika kwa minong'ono ya chumbani bila kujua nilikuwa nyuma nami nilisikia.
Mambo yale yale nilijua yameisha, lahaula kumbe bado yanaendelea.
Alimaanisha usiku ule wengi wasingejua lakini sisi tulipata taarifa mapema.
Nilichokisema kwako ni kile nilichosikia nyakati zile za usiku, ilikuwa siri lkn imeng'amuliwa mchana kweupeee!
Kwanza walikuwa wenzetu kama ujuavyo mwenye mali akitafutwa kwake asiwepo asiye na mali apatami.
Mandhari ile ile ambayo ni adui kwa mwenye mali kwa asiye na mali inakuwa ikulu yake.
Sasa nisikuchoshe.
Ila nakumbuka CDF pale Chato ulisema utamuona SSH ofisini kwa dokezo lile la awali, nami kiherehere moyo washindwa kutulia watamani kusikia ukisema siku ile ya salamu za mwisho, sijui jicho lile liliwaelekea wao?
Sasa wote tulikuwepo hata wamiliki wa sauti zile za minong'ono nao kama kwa mbaaali niliwaona,
Ikumbushe akili yangu kwamba SSH naye siku moja atasema alidokezwa lkn hatuna shaka naye ataweza kusema kupitia TBC yetu, siku hiyo atawaliwe na hekima maana atalitonesha jereha lililopona na imani itarudi kwetu tutakusanya fito na kuijenga upya nyumba yetu iliyobomolewa na wageni tulowakaribisha kwetu kwa muda, ingawa usalama wake utatakiwa kuongezwa maradufu.
Unajua wageni wale walikuja na ngamia wao, kwa bahati mbaya kilikuwa kipindi cha masika, kwahivyo siku zile mvua ikinyesha karibu kila siku, kwa huruma yetu tulimwingiza ngamia wao ndani ya nyumba yetu angalau kichwa chake tu, mwishome mwili mzima ukaingia ndani na kwa udogo wa nyumba ile wenyeji tulisukumwa kabisa hadi nje na wageni wale wakawa watawala nya nyumba zetu wenyewe.
Sasa tumekasirika tutatumia mijeredi kuwatoa nyumbani mwetu tuendelee kuwa wamiliki.
Jicho letu la hasira lilianzia pale kuokoa watu katika Mv Nyerere Ukara-Ukerewe, si unakumbuka ndipo nguzo za urafiki wetu zilianza kutetemeshwa na mtikisiko wa ardhi?
Ngoja nikukumbushe, si unajua zamani sana tulisafiri kwa kutumia punda kama safari yetu ni fupi?
Na kama safari yetu tungepitia jangwani ngamia wasinge ambatana nasi?
Na zaidi kama tungesafiri kwenda mbali zaidi si tuliwatumia farasi?
Sasa mbona wataka punda katika safari ndefu tena njia zako za jangwani umewaacha ngamia?
Kwenye safari zetu zote hatukuacha kikombe kilichovunjika mkono maadam hakivuji.