Video: Bingeni, Werema aonya Serikali moja mwiko

Video: Bingeni, Werema aonya Serikali moja mwiko

Mbona sasa wana dectate upatikanaji wa hiyo KATIBA? Kama hawataki wingi wa GHARAMA basi tuende SERIKAI MOJA, ama tukubaliane SERIKALI ya MAPINDUZI ndiyo iwepo hiyo moja ya kuongoza TAIFA.

 
Last edited by a moderator:
pakua ule ..... acha majungu mkuu
 
Huyo werema ni mnafiki,anasema lazima iwepo serekali ya mapinduzi zanzbr kwanini hasemi serekali yenye mamlaka kamili zanzibr?zanzibr serekali ipo wanachohitaji wazanzbar ni mamlaka kamili,kama serekali kuwepo basi iwepo ya tanganyika.
 
huyo werema ni mnafiki,anasema lazima iwepo serekali ya mapinduzi zanzbr kwanini hasemi serekali yenye mamlaka kamili zanzibr?zanzibr serekali ipo wanachohitaji wazanzbar ni mamlaka kamili,kama serekali kuwepo basi iwepo ya tanganyika.

usitupeleke unapotaka ,.inaitwa serikali ya mapinduzi zanzibar ,kwani uongo?
 
Huyo 'jaji' Werema anasema kuwa uwepo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (katika muungano) ni muhimu.

Umuhimu wake ni upi? Na vipi uwepo wa serikali ya Tanganyika?

Yaani hili linchi bana!!!
 
Anajitahidi kuleta fadhila kwa Mkuu wa Kaya ,lakini upande mwingine anachemka na analitambua hilo...
 
Kwanza Werema sio mjumbe wa Bunge la Katiba kwani huyu ni ex official na sio mbunge kamili, niwashangae mnaomsikiliza huku, huyu anapaswa kuwa nje ya Bunge la katiba , huyu ni mwanasheria mkuu wa Tanganyika kama Ana hadhi na wa Zanzibar Aitwe haraka ...
 
Hadidu za Rejea zilipotoka, hata upatikanaji wa katiba kwa jinsi watu na taasisi kama Bunge la Katiba zinavyopenda ukawa umefungwa pingu na kibaya zaidi hata Jaji Warioba na Tume yake wakaja na angalizo lao na kusema Madaraka ya Bunge Maalum ni kuboresha Rasimu ya Katiba na siyo kunyang'anya madaraka ya wananchi (act of popular sovereignty).

Kwa sasa tena amekuja Mwanasheria Mkuu wa Serikali na angalizo lingine la kuzuia kujadili Serikali Moja kwa sababu kufanya hivyo katika macho yake kisheria ni kuvunja sheria ambayo ndiyo msingi wa upatikanaji wa Rasimu ya Katiba.

Sasa hiyo Rasimu utaiboreshaje bila kubadili au kuviondoa baadhi ya vipengele?. Inakuwa kama neno uboreshaji ni kupitia vifungu na kuvikubali au kuvikataa lakini siyo kuviondoa, kuongeza au kubadilisha.

Sasa mantiki ya Bunge la Katiba ni nini katika eneo la taasisi inayojitegemea katika maamuzi yake nje ya Tume ya Jaji Warioba hasa ikichukuliwa kuwa hawa jamaa wanataka posho zaidi wakidai kuwa kazi waliyopewa ni muhimu sana kwa vizazi vijavyo. Hii inakuwa ni sawasawa na kuwa na chombo ambacho kazi yake ni rubber stamp.

Hapa ninaiona mantiki iliyokuwa inapigiwa kelele ya kuendelea kuwepo au kutokuwepo kwa Tume ya Jaji Warioba hata kipindi hiki cha Bunge la Katiba huku ikijikusanyia Tsh 500,000 kama posho za siku kwa kila mjumbe katika misingi ya kutoa ufafanuzi katika Bunge la Katiba pindi inapohitajiwa na wajumbe.

Tutaona na kusikia mengi.
 
Huyo werema ni mnafiki,anasema lazima iwepo serekali ya mapinduzi zanzbr kwanini hasemi serekali yenye mamlaka kamili zanzibr?zanzibr serekali ipo wanachohitaji wazanzbar ni mamlaka kamili,kama serekali kuwepo basi iwepo ya tanganyika.

mamlaka kamili ni kuvunja muungano tu... hamuwezi kuungana alafu hamtaki kuwa kitu kimoja
 
Back
Top Bottom