VIDEO - Bibi Afukuza Majambazi Kwa Maembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Bibi Afukuza Majambazi Kwa Maembe

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jul 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Jambazi akivurumishiwa mvua ya maembe[/TD]
  [TD]Hata maembe kumbe nayo ni silaha tosha, Bibi mmoja wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 80 amewatoa mkuku majambazi wenye silaha kwa kuwavurumishia maembe wakati wakijaribu kuiba pesa kwenye duka la binti yake.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Bibi huyo mkazi wa Massachusetts nchini Marekani alikuwa ndani ya duka la mwanae wakati wanaume wawili wenye silaha walipovamia na kumlazimisha binti yake atoe pesa zote zilizomo kwenye duka hilo.

  Bibi huyo aliyetajwa kwa jina la Otilia Martins alikuta mmoja wa majambazi hao akimlazimisha binti yake atoe pesa huku jambazi mwingine akiangalia usalama ndani ya duka hilo.

  Bibi Otilia aliwavalia njuga majambazi hao na kuanza kuwavurumishia maembe na kuwafanya majambazi hao watoke mbio.

  Bibi huyo alipigwa na kitako cha bunduki wakati alipomdaka shati mmoja wa majambazi wakati akikimbia kuepuka mvua ya maembe.

  Bibi huyo ingawa alivuja damu nyingi puani lakini aligoma kwenda hospitali kupatiwa matibabu.

  Majambazi hao baadae walitambulika kuwa ni Eduardo Torres-Lopez mwenye umri wa miaka 22, na Jesse DosSantos mwenye umri wa miaka 24.

  Majambazi hao walifunguliwa mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na kufanya ujambazi. Wametiwa mbaroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
  VIDEO - Bibi Afukuza Majambazi Kwa Maembe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...