VIDEO: Askari wa Usalama Barabarani akichukua Rushwa - Juni 01, 2016

Hiyo sio rushwa huko ni kupooza njaa na kusaidiana.....Wenye kula rushwa wako ofisini wapigwa na kiyoyozi.
 
Sasa ma transporter wote tuungane tuwakomeshe wa kwenye Mizani ya Uyole, Mbeya, Gari zisizozidi zinapigwa faini zilizozidi kila Gari bora utoe shs50,000.00 mpaka 100,000.00 unapeta, Hawa nao wamulikwe jamani.
 
mimi nawalia mingo wale wa pale kwenye daraja la mlalakuwa karibu na makao makuu ya jkt kawe..yaani wale washenzi wanachukua rushwa kama hawatafufuliwa yesu akirudi..
 
mimi nawalia mingo wale wa pale kwenye daraja la mlalakuwa karibu na makao makuu ya jkt kawe..yaani wale washenzi wanachukua rushwa kama hawatafufuliwa yesu akirudi..
Yaani nilikuwa na mpango huo huo, lazima nimfukuzishe mtu kazi pale, we ngoja tu
 
Rais naona bado hajawashughulikia hawa majahili - dawa yao ni kukwatwa hivyo viganja vinavyo pokea rushwa !!
 
Sasa kwani wangetaa kutoa hiyo Rushwa wakaandikiwa faini yao wakalipa wangepungukiwa nini?
 
Mke wangu bandika ugali naleta mboga.... wazeee wa fedhaaaa......
 
hii kitu bana inauma kama umeonewa na ni nzuri kama inakusaidia...#Rushwa
 
lengo Kubwa upandishwe cheo jamiiforums au, kwa mtadhamo wako wamepokea million ngapi yaan nchi hii ni shida yana Siku hizo ukimuona MTU kasimama sehemu muda mlefu uku town juwa kuwa kuna issue anataka ku-record ili asambaze kwenye mitandao. Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu badala ya kuwapiga picha watu wanaojisaidia stand za magari ya mwendo kasi.
 
Hiyo si ni faini huyo dereva anatoa kwa trafiki mtoa post acha umbea kuwaharibia wenzio kibarua Dereva hapo analipa fine na sio rushwa.Anyway uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na tukio hili
 
Askari wetu wakati mwingine unaweza kudhani akiona pesa akili zinahama kichwani. Hivi umati woote wa watu uliokuwa hapo hujiongezi tu kichwani ukaona mazingira hayaruhusu. Mbuzi wa hitima huwa hakwepi kuchinjwa.
 
Back
Top Bottom