VIDEO: Askari wa Usalama Barabarani akichukua Rushwa - Juni 01, 2016

Jun 3, 2016
1
7
Huyu ni askari anayesadikiwa kutoka katika kituo cha Urafiki, kilichoko Ubungo Dar es Salaam.

Alikuwa na wenzake wapatao wanne au watano, mmoja akiwa katika sare za jeshi pia, na wengine wakiwa katika mavazi ya kiraia. Walitega mingo katika makutano ya barabara ya Ubungo Maziwa na Barabara ya Morogoro. Walikuwa wakichukua rushwa kwa dereva wa bodaboda na magari. Mengine, jionee zaidi.

My Take:
Rais Magufuli anayo kazi kubwa sana katika mapambano dhidi ya rushwa. Ni lazima awafanyie kazi askari wa Jeshi la Polisi, kama kweli ana nia ya dhati ya kukomesha rushwa ndogondogo ambazo zinasababisha vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani zisizokoma.

Tafadhali saidieni kuisambaza video hii hadi iwafikie wenye mamlaka, wawezao kuwachukulia hatua askari hawa.

Nawasilisha.



Machi 31, 2016 kuna mdau alishadokeza juu ya tabia ya Askari jijini Dar kuchukua rushwa kwa njia ya kutopokea mkononi na kukulazimisha kupeleka "mzigo" kwenye gari mwenyewe:
Askari wa Usalama Barabarani eneo la Sayansi Kijitonyama Jijini Dar ni jipu.

Wanalazimisha uwape rushwa. Wamebuni namna ya kupokea rushwa, unaambiwa uingie kwenye gari (ieleweke hilo gari linakuwa la trafiki, muda mwingi linakuwa limepaki hapo), Ukiingia kwenye gari wanalock, unatoa rushwa unaacha kwenye gari, wanakufungulia unaondoka.

Mimi nimefanyiwa hivyo so nina uhakika ninachokisema.

Tutafika tu.
 
rushwa ni mbaya pia ni adui wa haki!
najua jamaa kibarua kitaota nyasi, sijui familia yake itakula nini! japo watanzania siku hizi wanafurahi sana wakiona mtumishi wa umma kapata matatizo kama haya (kutumbuliwa)

nafikiri tufikiri zaidi kwanini mtumishi wa umma anachukua rushwa,je mishaara midogo,ukosefu wa maadili ? tuje na suluhu ya tatizo hili la rushwa.
 
kwa serikali hii hawa si walisifiwa kuwa wanafanya kazi nzuri na kupandishwa vyeo? duh kweli kazi ipo,, sasa hapo kinachofuata ni Takukuru fanyeni kazi yenu,, siasa muwaachie wanasiasa
 
Ngoja ni suala la muda tutajua nani kilaza kati ya wale madogo na baba jane, ambaye kamzaa jane kilaza yawezekana genius kuzaa kilaza???
 
Hivi mfano mie nikaombwa rushwa na askari... halafu nikampa rushwa halafu nikawa nimemrekodi je? na mie nitachukuliwa hatua?
 
Sasa ngoja atumbuliwe huyo askari muone watakavomalizia hasira zao huko barabarani.Ukikosea tu umeandikiwa hakuna mjadala
 
MISHAHARA YA LAKI MBILI HAPO HAPO UOE HAPO HAPO USAIDIE WAZAZI WAKO ????? PUMBAVU,WAO WANAJILIPA MAMILIONI KWA MWEZI
 
inakuwaje pale bodaboda au dereva wa gari amekamatwa kwa kosa la faini ya sh50000 alafu akajitetea kwakutoa sh15000. je hapo wote watakuwa na makosa?.
 
Back
Top Bottom