VIDEO: Askari Magereza walivyoonyesha uwezo wao

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Askari Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 wakitoa maonesho mbalimbali ya Ukakamavu na ujasiri mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) alipofunga rasmi mafunzo ya kikosi hicho leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

 
Majeshi yetu yako vizuri sana.
Ni wakati sasa wa kuyatumia katika kuzalisha .

Ni wakati sasa wa kuwatumia malaki ya wafungwa walioko magerezani kuzalisha chakula kila kona ya nchi ili pasije kutokea tena uhaba wa chakula milele.
Uwezo wa majeshi yetu upo , nia wanayo na sababu ipo.

Kwenye medani za kivita majeshi yetu yanafanya vizuri sana lakini wakati huu wa amani wautumie kukuza uchumi na kujenga nchi kwa haraka.

Hii itapunguza upigaji na wizi unaofanywa na raia wasio wazalendo kwenye miradi mingi midogo midogo.

Hongera sana Askari wa Jeshi la Magereza kwa kuonyesha umahiri wenu kupitia mafunzo mliyoyapata.

Hao ni vijana wenye umri mdogo sana waliojitolea kuilinda nchi yetu. Ni uzalendo mkubwa wanaotuonyesha.
 
Back
Top Bottom