Victoria Group wamefia wapi?!

Victoria Group wamefia wapi?!

FACT:

Kundi hili lilianzishwa mwaka 1998 kama umoja wa kusaidiana kwenye kufiwa, kuuguza, kuoa na kusaidiana wakati wa kutafuta kazi.

Kundi hili liliitwa Victoria kwakuwa waanzilishi wake wengi walikuwa wametokea Kanda ya Ziwa (Mwanza na Mara).

Mwenyekiti wake wa sasa ni mtu wa Tanga wala sio Kanda ya Ziwa. Aliyekuwa Mwenyekiti kabla ya wa sasa alikuwa Mnyakyusa, mwingine alikuwa Mmasai, mwingine wa Morogoro, mwingine wa Moshi n.k.

Mpaka sasa kundi hili ni “Social Economic Group” ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga.
 
Bandugu,

Wakati wa utawala uliopita kuliibuka kundi maarufu lililo sheheni watu wa kada mbali mbali hasa kutoka kanda ya ziwa lililoitwa "Victoria Group"

Kundi hili lilihusisha Wafanyabiashara, wanasiasa, wanataaluma mbalimbali, matapeli wapigaji na watoto wa mjini, wanamuziki na vibopa mbali mbali wa makampuni binafsi na serikali nk.

Pamoja na mambo yote kundi hilo pia lilikua linatajwa kua na matumizi makubwa sana ya anasa!

Moja ya mikakati yao ilikua ni "Kumpachika" MTU mmoja (Mwanachama mwenzao) kushika moja ya nafasi za juu kabisa za uongozi nchini!

Rais aliyepita analifahamu vizuri sana hili kundi!

Hata aliyewahi kua Mwanasheria wa "Voda" baadaye akaja kuukwaa uwaziri wa "Dhahabu na Almasi" alikua mwanachama kindaki ndaki!

Hili kundi lipo? Ajenda yao ilifanikiwa kwa kiasi gani? Kwanini Mara baada ya "MTU kutoka kwetu" kushika hatamu halisikiki? Vikao vyao vinafanyika wapi sikuhizi?

Kwa wale watoto wa mjini kama Pasco wa JF watakua na taarifa zao tu.. Hebu tupeane updates mwenye taarifa vigogo na ma-Pdg hawa ?
Huu uzi wa kipuuzi, mbona magroup yako mengi tu!? Au kuna mtu analengwa ndo maana ya kuuanzisha!?

SupaHandsome tujuze unalenga nini kuanzisha uzi huu!?
 
Back
Top Bottom