Mkatavimeo
JF-Expert Member
- Jan 3, 2011
- 2,150
- 875
Mzee wa njaa mwaga ishu mkuu, watu wazifanyie kazi....
Nachukia sana mambo ya undugu maofisini, majitu yanaajiriwa hayana hata sifa mnaishia kuyafanyia kazi zao...shit!
Vicky Mtetema acha kufanya ofisi ya Under The Same Sun Mali yako......Peter Ash amekuweka hapo kwa kukuamini na sio porojo..Hiyo tabia ya kuita watu kwenye interview na kuchukua ndugu zako pamoja na jamaa zako ungeamua moja kwa moja kuwaweka kuliko kusumbua watu na kuwapotezea muda wao na tambua muda una thamani kubwa.
Iko siku na wewe utaicha ofisi hiyo na atashika mtu mwingine kwani ofisi hiyo ni taasisi inayoheshimika sana Duniani kwanini wewe Tawi la Tanzania unaliharibu kwa kuleta undugu kwenye ajira? Heshimu taaluma za watu na wewe utaheshimiwa.
Ukibisha tutatoa mambo ya ndani kwenye ofisi hiyo tunakuomba uache...Ile documentary isikupe kiburi sana naona kwasasa una nyodo nyingi kwa hako kacheo......
Naswasilisha.....Vicky tumechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa acha hizo.
mimi nataka hayo hapo kwenye bluu....aunasubiri yakukute ya mwakyembe ndo useme ukipona utasema???
acha hizo bana
KUWA NA AIBU wewe PASCO, wewe ni premium member hutakiwi kufagilia mambo ya hovyo hovyo. Haya mambo ya hovyo hovyo ndio yamefanya hii nchi isiendelee na wote tunaona utendaji mbovu wa mawaziri na wakuu wa mikoa waliowekwa kwa uswahiba na bosi wako JK...Wabongo kwa majungu, si mchezo!. Ile ni NGO tuu, aliyeileta Tanzania ni Vicky kupitia ile award winning yake ya mauaji ya albino akiwa BBC. Yeye ndiye anajua anataka nini. Ukitangaza kazi bongo, watajitokeza watu wana mavyeti ya kutisha lakini uwezo sifuri!. Kuna ubaya gani kuchukua the people you know wana uwezo hata kama hawana macheti!. Tuache majungu bandugu!. Majungu hayajengi!.
mwambie pasco anaongea kiupupukuwa na aibu wewe pasco, wewe ni premium member hutakiwi kufagilia mambo ya hovyo hovyo. Haya mambo ya hovyo hovyo ndio yamefanya hii nchi isiendelee na wote tunaona utendaji mbovu wa mawaziri na wakuu wa mikoa waliowekwa kwa uswahiba na bosi wako jk...
Utss kama ni taasisi serious lazima itakuwa na ant nepostism policy inayozuia kuajiri ndugu na marafiki katika organisation. Watu waliishafanya research wakagundua kuwa conflict of interests ziko kibao kama mnapeana ajira maswahiba. Au wewe pasco secretary
wako ni demu wako nini ndio maana huoni ubaya wa kuhire mashoga zako?
Nguo hutakata kwa sabuni.Mtoa mada ameambiwa kuwa alete ushahidi wa kuthibitisha madai yake kuwa Vicky amekuwa anapendelea ndugu zake kwenye kuthibitisha madai hayo mleta mada anamtaja mtu mmoja anayefahamika kwa ajina la Happy kuwa alikuwa msichana wa kazi wa Vicky na ameajiriwa hapo UtSS kama office attendant. Sasa angalia contradiction ya mtoa shutuma, kwanza kasema kaajiri ndugu zake , hivi katika Hirachy ya undugu kuna ndugu anaitwa Mtumishi wa kazi? Maana mtoa hoja anadai Happy alikuwa mtumishi wa kazi nyumbani kwa Vicky hivyo basi hii ina maanisha hata kama ni kweli Happy alikuwa ni mtumishi wa kazi hakuwa ndugu yake Vicky kinyume na madai ya mlalamikaji. Mbili mtoa mada kasema kuwa watu wameenda na vyeti vya degree lakini walikosa kazi. Sasa nauliza chuo gani Tanzania kinatoa degree za maofisi attendants? kama kipo unaweza ukathibitisha bila kuacha shaka kuwa katika hiyo interview ambayo ndugu yangu inaonekana ulikuwa umeomba na kupigwa chini kulikuwa na watu waliokuwa wameomba nafasi hiyo na walikuwa na sifa za kuwa office attendant.
Hata hivyo ningependa kumuasa mlalamikaji kuwa kila mtu hupenda kufanya kazi na mtu anyemwamini na anayemjua kuwa atafanya kazi inavyotakiwa. Vicky ndiye mwenye wazo la kuileta UtSS Tanzania, yeye ndiye mwenye Vision, anajua wapi anataka UTSS ifike, ndiye aliye na objectives za miradi ya UTSS, kwa hiyo basi yeye ndiye anayejua quality ya timu ya kufanya kazi nayo ili waweze kufikia malengo i-comprise watu wa namna gani. Nadhani kutokana na hilo Vicky anajikuta ana haki ya kuunda timu ya kumsaidia kutimiza malengo.
Ndugu yangu vicky ana uzoefu mzuri wa kufanya kazi katika mazingira mbali mbali na watu mbali mbali wenye tabia na mila zinazotofautiana. Vicky ana shule ya kueleweka, mwenye uzoefu na BBC (ukiacha mashirika mengine aliyofanyia kazi) wa zaidi ya miaka 20 (10 Akiwa based London). Vicky sio mtu w akujipendekeza. Vicky angekuwa mtu wa kujipendekeza kwa wakubwa angekuwa leo hata DC au RC. Vicky ni miongoni mwa watu waliokuwa wanatengeneza heading za maana zilizowafanya watu wakae karibu na redio zao kuisikiliza BBC. Vicky alikuwa akifanya interview na mkubwa yeyote lazima utaona content, na mra nyingi wakubwa walikataa kufanya interviews na Vicky. Mmoja wa watu ambao Mr. Clean aliwachukia Tanzania ni Vicky. Vicky ndio alikuwa wa kwanza kuchallenge sera ya shule za kata. Alitoka na documentary zenye data za kueleweka zilizoonyesha udhaifu wa sera hiyo na utekelezaji wake, na alitoa majibu mbadala na nini kifanyike. Aliwaconfront Mkapa pamoja na Mungai live juu ya suala la elimu TZ.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 Vicky ndio mtangazaji wa kwanza kabisa kujua na kuliweka wazi ukubwa wa tatizo la UKIMWI wilayani Makete. na hakutumia nafasi hiyo kama ambavyo mlalamikaji hapa anataka tuamini kuwa hujinufaisha mwenyewe kwa manufaa binafsi. Tuliona watangazaji waliofuata baada ya Vicky walikuja Makete wakatengeneza Documentary, wakaandika makala wakazitangaza, wakaanza kuomba michango ya watanzania, pesa hiyo mpaka leo haifahamiki kama ilifika Makete, sijawahi sikia vicky akiomba mtu ampe mchango kwa ajili ya waathirika wa UKIMWI ingawa ametoa misaada mingi sana. Tofauti na Vicky hao watu leo hii wamekuwa wakuu wa wilaya wengine Ma - RC na kibaya zaidi wameishau hata hiyo Makete (UKIMWI) iliyowatoa. Vicky mpaka leo hii amekuwa rafiki wa karibu kabisa wa watu wanaoishi na HIV huku Makete, Vicky amepambana sambamba na watu wanaoishi na VVU kuhakikisha kuwa haki zao zinatambuliwa, utu wao unaheshimiwa na kuwa watu wanapata matibabu na matunzo wanayostahili. Mpaka leo hii kuna waVVU wengi tu kutoka katika vijiji vya ndani kabisa makete waliofika na kupata kulala na kula na Vicky na yeye haendi na picha hizi au matukio haya hewani Vicky yeye huwasaidia watu huko huko waliko bila kudisturb life setting zao na akaacha watu waendelee na maisha yao huko huko waliko wakiwa wamebadirika positively. Sasa ndugu unasema angewachukua watu wenye ulemavua wa ngozi ili iweje, issue sio kuwaajiri katika NGO ya under the same sun, maana ukifanya hivyo mradi wako hautakuwa sustainable. Siku NGO hiyo ikifunga shughuri zake tanzania huyo mu-albino aliyeajiriwa hapo ataenda wapi? Anachofanya Vicky ni kuhakikisha kuwa kuna suluhisho la kudumu, sio kuwapa watu blanket na unga ukasema tumewasaidia waathirika kadhaa katika wilaya kadhaa. Mpaka leo hii Vicky ana watoto yatima makete wanaosoma kwa jina lake, lakini hatujamsikia popote akisema nasomesha yatima au watoto walio katika mazingira magumu.
Ndugu yangu hapa Tanzania kumekuwa na ubabaishaji mwingi sana, watu wana mavyeti ya kutisha ukiwapa kazi wanavurunda mpaka unashangaa huyu ndiye nilimuita kwenye interview? unashika kichwa na kujiuliza hivi huyu ndiye yule ameleta mavyeti mpaka nikashindwa kuyadownload kwenye e-mail? lakini kuna watu hawana vyeti hivyo unavyovitaka wewe wanachapa kazi kwa kwenda mbele. Najiuliza kama wewe au huyo ndugu yako angepata nfasi katika interview hii ungeleta malalamiko hayo kuwa bora angewapa nafasi hizo wenzetu wenye albinism?
Nakumbuka mwaka 2006 wakati wana JF walipokamatwa na Dola na kuwekwa ndani. Vicky Ntetema aliifanya ile story kuwa story kubwa ya BBC na kuwafanya wapigania haki mbali mbali dunia kusimama na kuwatetea akina Maxence, Vicky aliiona JF kama chombo mojawapo cha habari kinachopaswa kutambuliwa na kuheshimiwa. Na kwa habari za BBC wakati ule zilitufanya wote tujiulize what is this Jambo Forum, tukagoogle, tukaingia na baadaye tukajiunga. Kwa hiyio hii Jamii Forums unayoiona leo ina watu wengi sana wasingekuwepo hapa bila BBC kuifanya story ya kukamwatwa kwa akina maxence a leading story katika story zao za wiki ile.
Nadhani ndugu yangu hujamtendea haki Vicky kwa kumu-accuse kwasababu tu uliitwa kwenye interview au ndugu yako aliitwa kwenye interview ukitegemea kuwa ana vyeti basi atachaguliwa. Nadhani mtu aliyeweza kufanya kazi ya House keeping vizuri atakuwa ni ideal candidate kwa nafasi ya Ofiice attendant. Labda uwe na Hoja nyingine, na labda uwe na agenda iliyofichika la sivyo madai yako ni baseless, yasiyokuwa na facts za kuthibisha pasipo kuacha mashaka.