Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa. Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata.

KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni. Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii. “Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).

MAFANIKIO YAANZA Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano. Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.

MJENGO WA GHOROFA MBILI Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne. Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake.

MAGARI YAKE SASA Kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261. Ana Toyota Voxy- Noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16. Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130. Mara nyingi anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90. Pia mwanamama huyo ana gari aina ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25.

ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU Wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake. “Vicky amenunua mgodi wa dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari.

ANA SHAMBA LA EKARI 157 Utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba lenye ekari 150, Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la miti Kibamba, Dar lenye ekari 7. NI MFUGAJI Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.

ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA Katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.

KIPATO CHAKE KIKOJE?

Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.

AMFUNIKA ANNE MAKINDA Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake ipo Kijitonyama.

ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME Uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24. Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.

HI NDIYO CCM INAYOWATETEA MASIKINI NA WAKULIMA NAWANYONGE.
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz
 
Unatumia kigezo gani cha kufananishaje utajiri wa sugu na vick.
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz
Ufisadi usiutetee hivyo.....lazima tuhoji mkuu
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

wewe nae vipi jamaa kacopy toka uwazi usifikiri kila muda ni siasa.
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz
Mkuu sio kila kitu lazima ujibu ... some times kuwa silent ni busara zaidi kuliko kutetea kila kitu kinachostahili kujadiliwa ...
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

Naona hakuna tatizo nadhani yeye kawakilisha tu ripoti toka gazetini
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

Le Mutuz Sugu anautajiri gani zaidi ya nyumba iliyoko mby na gari moja ya kutembelea
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz
Kichwa chako we jamaa cjui kikoje.....Yaani sugu naye anautajiri...loh! Haya mzee wa lagos
 
SafI ametumia fursa ipasavyo....kutoka Ualimu hadi BOT then Bungeni mpaka kuwa Bilionea ndani ya miaka mitano.!!!

Ukiuliza amepataje mali hizo....jibu rahisi tu ametumia fursa.!!!
 
Serikali ya Tanzania imelala pamoja na tiss yake. Unapopata habari kama izi awe sugu awe nani ni lazima kufuatilia na kuzifanyia kazi hata kama Kamata anatembea na rais lakini ijulikane amepataje utajiri huo. Na kujua je hizi/hizo mali alizonazo ni zake na amezipataje. Kamata amekuwa afisa uhusiano wa bot na 2010 akawa mbunge, kwa mali inayozungumziwa ni karibu bilioni mbili. Jamani wadanganyika wapo waliokaa bungeni zaidi ya miaka 30 lakini hawana utajiri wa haraka kiasi hicho. Acheni maneno inatakiwa serikali ifanye kazi kutokana na habari ndio maana ya kuwa na waandishi wa habari. Huyo sijui Lemutuz hana lolote hawezi kusema kuwa mwacheni bila kufuatiliwa. Hivi wewe Lemutuz umeishi kweli Marekani au ulikuwa upo upo tu pale Marekani lakini ujui ulimwengu inakwendaje. Hapa ndipo ninapoilaumu tena serikali kutumia pesa za walalahoi kuwapeleka watoto wa wakubwa kusoma nje. Na kurudi kichwa ikiwa tupu kama huyu. Nilitegemea angekuwa mstari wa mbele kukemea na hata kutoa ushauri kumbe kichwa ni pumba kabisa
 
Back
Top Bottom