Slaa amechemka sana kwa kutoa kauli hizi mbili, ya Maaskofu wa Katoliki kununuliwa na ya magari kutumika kupeleka watu Jangwani. Natoa sababu kama ifuatavyo: kwa kusema maaskofu Katoliki wamenunuliwa inaweza kuchochea makundi mengine ya kidini kuunga mkono upande wa pili ili kudhibiti hila za walionunuliwa. Kwa kusema magari yalisomba watu kutoka nje ya Dar inamaanisha kuna wapambe wengi wanaoweza kukubali kuacha kazi zao kuja Dar kujaza Jangwani kwa ajili ya Lowasa. Je, watu wa aina hiyo si ni kura za uhakika kwa Lowasa? Mimi nadhani angetumia kauli ya wanywa viroba ningeona anasaidia upande wa pili maana hao asilimia kubwa hawatapiga kura. Hizi point mbili za Slaa mimi naziona ni fake sana.