Vibanda vya Machinga Complex vyabomolewa, Machinga wahaha



!
!
Poleni sana jamani.......
 
Hilo jengo limeshindikana kwa biashara ya machinga, serikali ingegeuza tu ofisi za idara mbalimbali
 
Ule ni upoyoyo, mambo mengine hayahitaji uwe na shahada ya uchumi kuyatambua.
Eti mnajenga vibanda nje ili mpate wateja kiurahisi huku mmejengewa safe & planned place.
Wateja hawafuati mahali bali bidhaa. Wote wakiwa kwenye vizimba wateja lazima tutawafuata huko.
Kama wanaogopa kodi hiyo ni kesi nyingine, waombe punguzo.
Hakuna jambo gumu duniani.
Tatizo liko kwa wachache ambao waliwazibia wenzao wateja kwa kupanga bidhaa nje.
Wakirudia tena kukaa nje huku ndani kuna nafasi wahamishwe kwa virungu na kuwekwa lupango ili waelimike.
 
Hii mijitu inategemea kodi za machinga hadi kununua karatasi za chooni halafu inatoa maamuzi ya ajabu hata mbuzi hawezi kufanya.

Punguzeni roho mbaya hata sisi watu wa chini tuna majukumu.
 

Mnaopita barabara za Uhuru, Kawawa, Nyerere maeneo ya Machinga Complex jijini Dar badilisheni mwelekeo, barabara hizo zina msongamano mkubwa wa magari kutokana na Machinga kuchoma matairi kwenye jengo la Machinga Complex baada ya vibandao vyao vilivyo jirani na jengo ilo kubomolewa.
 
Hakuna kinachoshindikanaga mkikaaa mezani wanaofanya mambo Yafike this FAR wanashangaza
 
Hawa machinga wengi ni watu waliokosa elimu na wenye elimu pia wameficha taaluma zao na kujiingiza katika kundi la wapumbavu.
Mmejengewa jengo zuri na lililopangwa kitaalamu kwa ajili yenu hamtaki kwa sababu ambazo zinatatulika kwa urahisi sana.
-Kama tatizo ni kodi kubwa, ni suala la kuongea na uongozi wao wangepeleka malalamiko halmashauri, kwa ninavyojua Makonda wa Dar mpenda sifa angelitatua haraka.
-Kama tatizo ni wateja hawataki kuingia ndani, hili suala ni la uongozi wao wa machinga kutoa shinikizo wafanyabiashara wote waingie ndani na nje hatoruhusiwa mtu labda tu vizimba vyote viwe vimejaa. Wateja huwa hufuata bidhaa zilipo, lazima kama wateja tungeona fahari kuingia ndani kufuata bidhaa.
Wapigwe na virungu, mabomu ya machozi na lupango waingizwe baadhi yao ili wawe wafuata sheria na kanuni.
 
Hahaha jamaa kadhamiria kuwaondosha watu Dar na kuwarudisha kijijini, basi bhana ngoja uchumi uzidi kukua
Sometimes tuwe serious....kwanini biashara isifanyike ndani ya majengo?
 
Mkuu kwa Tz bidhaa ndio umfuata mteja...hatuna tamaduni ya kufanya shopping so tunanunua tukiona kitu barabarani kikakuvutia
 
Acha waungane na wenzao wa Mwanza kuisoma namba.
 
mimi ni furaha bila haya kutokea akili za watanzania haziwezi kufunguka....hii mijitu ndo utaona inapigia debe chama chakavu kiendelee kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…