Viatu vya dola 12,000 vya Jose Chameleone

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Viatu vya dola elfu 12 vya Jose Chameleone

160204171311_jose_chameleone_624x351_jchameleone.jpg


Viatu vya dola elfu 12 vya Jose Chameleone
Wewe ukijikakamua zaidi unaweza kutoa pesa ngapi kununua kiatu....?

Haya basi ,mwanamuziki maarufu kutoka Uganda Jose Chameleone amenunua jozi moja ya kiatu kwa kulipa dola elfu 12 na nusu .

Sasa wengine wanadai eti anajionyesha kuwa anazo.

Lakini yeye anasema ameamua kuzawadi miguu yake!

Muimbaji huyo wa wimbo wa ''Wale wale, waliobarikiwa na mungu '' anasema sio majivuno kamwe bali ni njia yake ya kumshukuru mungu kwa kumjalia na kumpa uwezo kama huo.

Wimbo huu wake wa hivi karibuni umetazamwa na watu zaidi ya milioni moja laki tatu katika mtandao wa Youtube kote .

Juzi alipokuwa ziarana nchini Kenya, aliwaacha watu vinywa wazi kwani aliweka mtandaoni picha ya vyatu vyake aina ya Nike Air Mag.

Jozi hio ya viatu vya nike alinunua kwa dola 12,500 za kimarekani.

Hebu fikiria Chameleo ka nunua kiatu kwa jozi moja kwa pesa sawa na milioni moja na laki tatu za Kenya au karibu milioni 26 za Tanzania.

Mwenyewe kasema anajipa raha, ''jifurahishe ungali hai'', Chameleoni anasema.

Amefafanua kuwa anarudishia miguu yake shukran ''kwa kusimama naye'' na kumuwezesha kufika alipoa sasa.

Chameleon anakumbusha kuwa miaka minane iliyopita nusura awe kiwete kutokana na ajali mbaya.

Sasa amepona na pesa ziko ''kwanini nisishukuru miguu yangu ?

Kwa mahasidi wake wanamzomea eti anajionyesha na kufuja pesa.. Chameleon anawapa ushauri kuwa ikiwa hawawezi kutoa dola elfy 12 mia tano kununua kiatu . Basi wachina wanauza viatu bei rahisi sana...wasimuonee sooo wakanunue viatu saize yao mali ya wachina

Chanzo: Viatu vya dola elfu 12 vya Jose Chameleone - BBC Swahili
 
Hongera yake...lkn asisahau kutoa zaka na sadaka...
ameshajibu hiyo,ana chameleone foundation kazi yake ni kutoa zaka na sadaka,viatu kanunua kwa ajili ya kuitukuza miguu yake iliyotaka kuvunjika alipodondoka toka ghorofani akiwa usingizini bongo.
 
Chameleon anakumbusha kuwa miaka minane iliyopita nusura awe kiwete kutokana na ajali mbaya.

Sasa amepona na pesa ziko ''kwanini nisishukuru miguu yangu ?

... financial indiscipline changanya na bangi
 
Ahhahaha eti wakanunue china
Wasanii wana tabia ya kuongeza tarakimu wanapotaja kiasi cha pesa walichotumia kufanya kitu flani. Kwamfano utakuta msanii anaropoka nimetumia zaidi ya 100m kutengeneza hii video kumbe uongo. Kama ni kweli kanunua kwa $12000 basi hongera kwake
 
Mtu masikini siku zote hapendi kuona mtu anafanikiwa au kufaya kile asichoweza sababu ya unasikini wake
 
Back
Top Bottom