Viashiria muhimu vya kifedha kutoka kwenye taarifa ya kifedha ya CRDB kwa robo ya pili ya mwaka 2025 (Q2 2025) - Unaudited Financial Statements)

Viashiria muhimu vya kifedha kutoka kwenye taarifa ya kifedha ya CRDB kwa robo ya pili ya mwaka 2025 (Q2 2025) - Unaudited Financial Statements)

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
119
■ Faida baada ya kodi (Q2 2025): TZS 346 Bilioni, ikilinganishwa na TZS 275 Bilioni kwa Q2 2024.
📈 Imeongezeka kwa 26% – hii inaonyesha ukuaji mzuri wa faida ya kampuni.
■ Interest Income (Mapato yanayotakana na riba za mikopo) Yameongezeka hadi TZS 904 Bilioni kwa nusu ya mwaka (Jan-Jun 2025), kutoka TZS 719 Bilioni mwaka jana.
■ Mapato yasiyo ya riba (Non-interest income): Yameongezeka hadi TZS 354 Bilioni, ikijumuisha ada za miamala, makato na faida kutokana na ubadilishaji wa fedha za kigeni.
■ Mikopo kwa wateja (Total Loans): TZS 12,250 Bilioni, ongezeko la 29% kutoka mwaka jana.
■ Amana za wateja (Total Deposits): TZS 13,936 Bilioni, ongezeko la 38% kutoka mwaka jana.
■ Loan-to-Deposit Ratio (Uwiano wa mikopo na amana): Iko kwenye 90.1%.
■ Jumla ya Mali (Total Assets): TZS 19,707 Bilioni, ongezeko la 32% kutoka TZS 14,966 Bilioni mwaka jana.
■ Mikopo chechefu (Non-Performing Loans - NPLs)
NPL Ratio: Imepungua hadi 3.0% kutoka 3.3%, ni dalili nzuri ya usimamizi bora wa mikopo. [ BOT anaelekeza iwe chini ya 5%].
■ Earnings per Share (EPS): TZS 66 kwa robo ya pili, ukilinganisha na TZS 56 kwa kipindi kama hicho mwaka jana.
➡️ Hii ni habari njema kwa wawekezaji kwani inaonyesha uwezekano wa gawio zuri zaidi.
■ Cost to Income Ratio (CIR) - Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato: 43% (Benki inajitahidi kupunguza gharama za uendeshaji, BOT anaelekeza iwe chini ya 5%).

Valuation Metrics:
● Bei ya sokoni: 1000 kwa kila hisa.
● NAV: 914
■ PB ratio(Uwiano wa bei ya hisa ya sokoni na bei ya vitabuni -NAV): × 1.09.
■ PE ratio (Uwiano wa bei na pato kwa kila hisa); Tuki - assume EPS ya robo zote ni 66, PE ratio inakuwa ni x 3.78.
■ Return on Assets (Mchango wa assets za kampuni kwenye faida): 5.2%
■ Return on Equity (Mchango wa mtaji wa wanahisa kwenye faida ya kampuni): 29.0% - Benchmark ni Return ya bond ya miaka 10 ~ 14%.

GODFREY DENIS
0763 721 523 (WhatsApp).
 
Back
Top Bottom