'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Uzi ulioandikwa na agents wa Shetani kwa nia ya kupotosha ukweli!?Evolution is fake science which cannot be proved by scientific research and experimentation,so it's rubbish.
Mfano Vestiges kama vishimo vya macho kwenye samaki wasio na macho deep sea kwenye giza, wana fake vipi??
 
Mfano Vestiges kama vishimo vya macho kwenye samaki wasio na macho deep sea kwenye giza, wana fake vipi??
Mkuu sijui niongee vipi,evolution is fake science because it cannot be proved by scientific research and experimentation.Nadhani tuishie hapo.
 
Mkuu sijui niongee vipi,evolution is fake science because it cannot be proved by scientific research and experimentation.Nadhani tuishie hapo.
Kwahiyo hao samaki wamekuwa forged? Ni fake? Appendix kwenye tumbo lako ni fake, haipo? Mifupa ya miguu kwenye nyangumi ni fake?
 
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.

Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.

Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!

=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================

Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
=============================

=================================
Update: 27/08/2021
Mifupa ya nyangumi mwenye miguu ‘dating millions of years ago’ yapatikana.

View attachment 1912340
_______________________________
WaChina ni WaAfrika waliohama na kubadilika kutokana na mazingira


kufikirika. haya nayo ni maarifa lakini ya hovyo
 
Umesema kuwa Kama kiungo hakitumiki hupotea chenyewe.
Swali: Ni vipi Hawa masista na mapadre ambao hawajamiiani/hawazai. Je mfumo wao wa uzazi unapotea mwilini mwao? Yaani nyeti zao hubaki kwaajili ya kukojoa na kunya tu?
Hao ma padr si wanapiga punyeto, na masista wanasugua visimi so , viungo vyao vya uzazi vitabaki vikifanya kazi
 
Maisha ya ulimwengu is about evolution.
Mfano mtoto akiwa anayonya ziwa la mama yake Ila atakapo Anza kuota meno , mama ata muanzisha kunywa uji , na baadaye Meno yakiongezeka, mama ana mbadilishia chakula, ubwabwa laini na nyama ana mtafunia mpaka atakapo atakapo komaa.

Mfano uvumbuzi wa ndege, ukiufatilia historia yake ,kama ni wewe ungekuwepo kipindi hicho uzingekuja Amini Leo , kungekuwepo na ndege yenye uwezo wa kubeba abiri mpaka 500.

Angalia wamasai wa kipindi tz inapata Uhuru walikuwa morani wanawinda Simba kama ni jambo Lao la kukamilisha mila za kuwa morani .
Lakin Leo wamasai wamezuiliwa wasi wasi wawinde Simba Kwani, Simba wengi walipungua, Sasa Simba wameongezeka mpaka watalii wanapewa kibali cha kuwawinda ili kuweza Ku balance food chain.

Hii itawapelekea morani wa kimasai kukosa ushujaa kama Zamani, tunaona morani wanasuka nywele Huku mjini, Wana Kula chips yai, hawali Tena nyama isioiva Sana na maziwa mabichi , baadaye miaka 100 , Hata wamasai hawatafaa kuwa walinzi, kwani wengi watakuwa wazembe wenye vitambi.

Tunaona katiba mbovu ya tz na CCM ikiongoza nchiki kichenzi ,
Hii imepelekea kuwa na vuguvugu la kudai mabadiliko Kwa nguvu Sana, pengine wao CCM wanaamini wataongoza tz 🇹🇿 hivihivi , lakini kutokana na hasira za wananchi juu ya Katiba mbovu na CCM ikiongoza nchiki vibaya, huwenda pakatokea mapinduzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom