Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,527
- 14,399
1. Pundamilia anavutia lakini anaishi na wanyama porini, Punda wa kawaida havutii lakini anaishi majumbani na watu.
2. Huyu Punda wa kawaida uwezo wake wa kubeba mizigo (kuchapa kazi) ndo umempa heshima ya kuishi na watu mujini.
3. Kwa mfano huu tunajifunza kwamba katika jamii ya leo kinachokupa heshima ni kazi unayofanya, siyo uzuri ulionao ndiyo maana watu watakuuliza unafanya kazi gani ili waone heshima ya kukupa.
4. Kazi ni kipimo cha utu. Hutaki kazi kaishi porini na Pundamilia. Unataka heshima fanya jambo la heshima.
5. Binadamu hajawahi kuheshimu mtu, anaheshi alicho nacho mtu!
6. Usipojituma kufanya kazi sura yako ya malaika, shingo ya upanga, macho yako ya golori, kiuno cha Ray C, miguu ya bia, rangi ya Mtume na muondoko wa twiga vitakupa pesa ya kula na kwenda saluni tu; ukitaka pesa ya maana kachape kazi.
7. Kufanya kazi ni kushiriki uumbaji wa Mungu katika ulimwengu unaoishi. Hata kwa nyie vijana wangu msipiganie uhandsome, piganieni kuchapa kazi.
8. Ukichapa kazi utapata maisha, ukipata maisha utakuwa handsome automatically alisema Diamond wa Tanzania.