Hahaha ila kweli..hata mimi wazazi wangu walikuwaga top three muda wote! Na sijawahi kuona matokeo yao...naamini tu!
Baba yangu alikuwa anapenda sana kutufundisha. Pamoja na ukali wake lakini ilitusaidia sana.
Kwa mfan hesabu..alikuwa anapenda kusema "Hesabu ni mchezo wa namba...It is just a game of numbers!" Ukipata swali anafurahiiiiiii basi na wewe unajiona bingwa kweli kweli!!!
Tunasoma tukimaliza tunaimba..infact, kipindi pekee tulikuwa tunamfurahia ni wakati akitufundisha tu maana huwa hachapi...ila mkimaliza hapo babaa...dah mara bustani, mara kazi za ndani, ng'ombe, ukitaka kucheza subiri mpaka uende shule! dah...
Umenikumbusha mabli na sayansi kimu...hivi hili somo siku hizi halijafutwa? Tulijifunza mambo mengi sana mazuri them dayz!!!