Verify you are not robot!!

Asante Mkuu hapo sasa kwa maelezo haya nimeelewa, kumbe robot lina uwezo wa kujibu kifasaha tena kwa haraka ila kwa sababu linajibu kimashine ndio maana linagundulika, hatari sana
 
Sometimes ni kwa usalama wa website account.. mfano ku recover email kwa 2 step verification n.k. binafsi sioni tatizo sana
Sio tatizo lakini usipokua makini ukikosea unakwamia hapohapo wakati taarifa zako umeingiza vizuri tu
 
Asante Mkuu hapo sasa kwa maelezo haya nimeelewa, kumbe robot lina uwezo wa kujibu kifasaha tena kwa haraka ila kwa sababu linajibu kimashine ndio maana linagundulika, hatari sana
Ndio, Kwa mfano kujibu kama hizo cross walks lenyewe linaona zote Kwa pamoja na kujibu ndani ya sekunde moja. Hiyo inakuwa alarm kwamba huyu sio binadamu. Na hiyo movement ya kamshale ka kompyuta binadamu Hana uwezo WA kuanyosha lazima apinde kidogo na spidi itapungua anapoclick mahali au atapitiliza kidogo na kurudi. Lakini robot linaenda Kwa spidi Kali na straight. Ingawa nasikia siku hizi na yenyewe yanafundishwa tabia za binadamu Kwa kujifanya kusita na kupinda Pinda lakini litadakwa hapo kwenye kujaza vitu ambayo binadamu haoni lenyewe linaona, litaingia kichwa kichwa linajaza na ndio linadakwa hapo hapo.
 
Sawa,Hivi hata hilo swali lenyewe "verify you are not robot" pia si linaulizwa na haohao bots ila tu linakua la ule upande mwingine au?
Ndyo nayo ni mifumo ya kiautomatic, lakin mara nying hua inaulizwa kama umeserch vitu ving kuliko kawaida au umelog in kwenye account several times au unataka kufungua account asa inaulzwa ili kuzuia account fake au udukuzi ndani ya mtandao. Ndo mana hua inauliza hivo . Au ikizidiwa sana hua inasema "I'm not a robot"
 
Vipi kwa site zinazotumia cloud flare ina msaada kuzuia robot?
 
Kuna clip mtaalamu mmoja alikua anaeleza kwamba, siku hizi ukivlick tu kibox inachapa tiki, haina haja ya kwenda kama zile crosswalk au magari,

System inatambua robot na binadamu kwa aina ya touch, robot linatouch kama mashine halikosei angle hivyo linagundulika kwa usahihi wake
 
Ni sawa na unaenda kuomba kazi wanakwambie cheti cha kuzaliwa kiwe katika viambatanisho. Hawaamini kama kweli ulizaliwa
 
Ok kumbe hivyo ndivyo ilivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…