Vengu apelekwa India (Apolo) kwa matibabu zaidi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Hatimae maombi ya wengi yametimia sasa kijana wetu vengu amekula pipa
kuelekea hukooooo appolo kwa wengi na wachache mlio dar ...habari zinasema
kijana yuko na wasaidizi watatu akiwemo dk anaemsaidia akiwa huko

ukiwa kama mtanzania sla zako ni muhimu zaidi baada ya kuomba hili tumwombee
perdiem alizopewa zisimkatikie akiwa bado anauguzwa huko

kila la kheri br vengu
polen sana kwa wasaanii na watanzania kwa kufiwa na mzee wetu wa siku nyingi kwenye usanii
 
Ni kweli kwani nami pia nimesikia habari za Vengu kufanyiwa mpango wa kwenda kupata matibabu zaidi nje ya nchi, tunawashukuru wale wote waliofanikisha ama wanaoshughulikia mpango huo kwani huko ndiko kujali tuachane na zile tabia za kuchanga mahela kibao wakati mtu ameshafariki ilhali tulikuwa na nafasi ya kumsaidia kwa matibabu bora ingali yu hai, Mungu akutangulieni nyote mnaomsaidia br Vengu.

Kuhusu Mzee Kipara ni habari za kusikitisha ila Tunamuomba Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi. Amina.
 
Vengu ndio nani?

Ni msanii wa kundi la Ze orijino komedi(alikua na kina Masanja, Joti, Mpoki etc) Yeye hajaonekana muda mrefu kidogo ila alikua akiigiza mara nyingi kama mchaga flan na pia aliigiza wimbo wa 20 percent-tamaa mbaya. Kama hujamuelewa mpaka hapo basi, sina msaada zaidi.
 
Kwa kweli naupongeza uongozi au hatua zilizofanywa kumpeleka huyo kijana India kwa matibabu, lakini roho inauma kuona kwa nini asingeanza Mzee Kipara ukichukulia yeye alianza kuumwa, na kama usanii vyovyote itakavyokuwa Mzee Kipara ametumikia sana jamii kwani tangia enzi za Mchezo wa radio na Radio Tanzania Daressalaam, enzi hizo nikisikia sauti naogopa. Mungu amjaalie Vengu apone arudi kwenye kazi, na amlaze Mzee Kipara pema peponi Amen. Ni maoni tu, hakuna suala la kutoa mapovu.
 
Mungu msaidie bro Vengu...fanya kitu kwa hili tu,ili nizidi kukusifu.Shikilia uhai wa Bro Vengu kwenye mikono yako yenye nguvu.
 
Kwa kweli naupongeza uongozi au hatua zilizofanywa kumpeleka huyo kijana India kwa matibabu, lakini roho inauma kuona kwa nini asingeanza Mzee Kipara ukichukulia yeye alianza kuumwa, na kama usanii vyovyote itakavyokuwa Mzee Kipara ametumikia sana jamii kwani tangia enzi za Mchezo wa radio na Radio Tanzania Daressalaam, enzi hizo nikisikia sauti naogopa. Mungu amjaalie Vengu apone arudi kwenye kazi, na amlaze Mzee Kipara pema peponi Amen. Ni maoni tu, hakuna suala la kutoa mapovu.

Amawai kuipigia kampeni CCM?
 
Back
Top Bottom